SHAMANIZ AWACHA MUZIKI KWA MUDA HUKU DOGO RICHY NA LYPSO WAKIJIPA MOTISHA!!!


Baada ya kuvuma na vibao motomoto na kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti.Binti msanii niliyemsikia kwa mara ya kwanza kwa wimbo NIMEZAMA alikuja wazi hapo jana na kuongea hadharani kuwa ameupiga teke muziki. Shamaniz aliyevuma kwa kibao kama romeo and juliet na vinginevyo aliandika haya kwenye ukurasa wake wa facebook....."Nimekuwa nikiwaza sana na nimeamua kujipa likizo kiasi,yaani naacha kuimba kwa muda.nahitaji kuangalia maswala kadhaa ili niweze kujisimamia pasipo na kufanyiwa bure..to all producers whom i have worked with,presentersand my sweet fans thank u 4 ur time n support till we meet again love u all and God bless you...." 
Imebainika wazi kuwa Shamaniz amewacha muziki kwa muda ili afanye maswala yatakayompatia hela za kulipia studio !! Huku Shamaniz akiongea hayo Lypso na Dogo Richy wanaobobea kwenye sanaa ya pwani na Kenya nzima kwa jumla walijitokeza na kunena haya kupitia kurasa zao za facebook....DOGO RICHY "I say wasanii kibao najua wengi mnatamani kuwacha mziki, maybe umeimba sana hakuna mafanikio,umefanya kila juhudi na bado haujafaulu..i say hakuna safari rahisi chochote kile duniani kiko hivyo so kaza buti na umuombe MUNGU sana amini sote tutafanikiwa." Naye LYPSO alikuwa na haya ya kusema...."Kuna siku nilitamani kurekodi japo niskie sauti yangu i worked hard nakurekodi samantha nikatamani kujiskia kwa radio nikafanya juhudi na kama kweli nikaweza kujiskia nikatamani kujiona kwa tv na bidii nikazidisha na nikaweza kudhibitisha hilo na kutangaza uwezo wangu kwa taifa kiukweli safari yangu ya mziki imekua ikinikuza dogo dogo na hua nashukuru kwani ni size yangu i sing within ma lyfe...." Ni dhahiri shahiri kuwa sanaa ya muziki hasa ya pwani imejawa na changamoto za kila aina na kweli inahitaji uvumilivu.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA