Breaking news, Msanii Fat-S ahusika kwenye ajali ya barabarani
Msanii Salim Mwinyi Fatty S Anauguza Majeraha Baada Ya Kuhusika Ya Katika Ajali Ya Barabarani. Ajali Hiyo Ya Basi Ilitokea Masaa Ya Asubuhi Wakati Basi Hilo Lilikuwa likitokea Jijini Dar es salaam Kuelekea Hapa Mjini Mombasa. Kulingana NaWalioshuhudiaAjali Hiyo Basi Hilo Liliacha Njia Na Kupinduka na Kusababisha Vifo vya watu Wawili pamoja na Kujeruhi abiria 10. Ajali hiyo ilitokea katika Eneo la Mkata na Goba Barabara Kuu ya Chalinze Segera.
Hata Hivyo Fatty anaendelea vyema Ikizikngatiwa hakuwa Amejeruhiwa Vibaya Sana Vile.
Si Kitambo Ndani Ya Mwaka Huu Fatty Alihusika Katika Ajali Nyingine Ya Pikipiki Nakumia Mguu. Aidha Fatty S Alikuwa Nchini Tanzania Kikazi Na Duru Za Kuaminika Nikuwa Alifanikiwa Kuandikisha Kandarasi Ya Miaka 10 Chini Ya Uangalizi wa Promoter Mkubwa Afrika Chief Kiumbe. Hata Hivyo Kwa muda Huo Akiwa Nchini Humo Alifanikiwa Kufanya Kazi Sio Chini Ya Tano Zingine Akiwahusisha Rich Mavoko, Mr Blue Nawengine Wengi Wakali Wenye Sifa.
Kama Pwani Usanii tunamtakia kupona kwa haraka
Comments
Post a Comment