DAZLAH: SIKUAMBIWA NA MAMANGU NINYOE DREADS NA MIMI SI MSANII WA CANDY N CANDY
Mkali wa miondoko ya muziki wa pwani, Kiduche almaarufu Dazlah amekuja wazi leo hii kuweka mambo wazi. Kwenye show ya mashavmashav alipohojiwa na presenta Eric Gates, msanii huyo alikana kuwa mamake mzazi ndiye aliyemwambia anyoe dread.
Uvumi ulikua eti Dazlah amemsahau Mungu na haendi tena msikitini ndiposa mamake akaingilia kati kwa hasira na kumwambia amrudie Mungu na anyoe dread aende msikitini kusali. Dazlah aliyapinga hayo na kudai ilikua hiari yake ya kugeuza image ndiposa akanyoa.
Vilevile msanii huyu amevunja madai ya kuwa bado yupo candy n candy records. Dazlah alisema kuwa alitoka CandynCandy na hafanyi kazi tena na wao ila huwa anaweza shirikiana na wao kupitia makubaliano fulani."Naweza fanya kazi na CandynCandy ila hawajanisajili" alisema Dazlah.
Comments
Post a Comment