KUTANA NAYE DULLY DA BROWN


JE DULLY DA BROWN NI NANI?
Dully da brown ni msanii ninayewakilisha Lamu na ni mkaazi wa kisauni.
ULIANZA KUFANYA MUZIKI LINI?
 Nilianza kupenda mziki toka premo hadi 2007 nikaanza kurekodi studio iitwayo Mo-45 mikononi mwa produza Kkroniq 
TUTAJIE BAADHI YA NYIMBO ULIZOWAHI KUZIFANYA
Nilifanikiwa kufanya ngoma kama, please binti, kijana, umbo lako, kisha nikaacha muziki mpaka 2011 ndipo nikajafanya mziki kwa studio JungleMasters ngoma inayoitwa 'msela' nikiwashirikisha Ommy na Kibery maujanja iliyofany­a vyema zaidi.Baada ya hapo nikakimbilia kwa produza Totty...ambapo ndo nilikita na kufanya ngoma ukapera na 'ambacha ukucha' inayovuma kwa waswahili wote.Vilevile niliamua kujitosa kwa mduara ambayo nilimshirikisha presenta wa pilipili fm maarufu kama Auntie Lyloo...inayoitwa 'Uchekechee' yani inazidi shika chati nashukuru" MTINDO WAKO WA KIMUZIKI NI WA KIPEKEE,UNAIMBA LUGHA YA KIBAJUNI KWENYE CHORUS ZAKO NYINGI. 
Yap iliyonifanya mpaka nikaanza kuleta chorus za kibajuni ambayo ni asili yangu ni wakati nikienda Lamu kuperfom jamaa walikua hawaamini mimi ni mbajuni ndio maana nikawaletea hisia za uswazi.
TUTAJIE BAADHI YA NYIMBO ZAKO ULIZOIMBA MTINDO HUO. 
Ambacha ukucha na uchekechee nkono... Wamekubali sasa hadi disco vumbi wanakata mauno.
JAMBO LA MWISHO UNGELIPENDA KUWAAMBIA MASHABIKI? 
Yeah,watarajie vitu motomoto vya kiuswazi mwaka huu!

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA