TOP SITA:RADIO SHOW KALI MKOANI PWANI ZINAZOKUZA VIPAJI VYA MUZIKI WA PWANI.


6. CHACHAWIZA YA BAHARI FM.
Show hii inayopeperushwa angani na presenter Farida Ali huanza saa saba mchana hadi kumi jioni. Farida huwahoji wasanii na kucheza muziki wa pwani japokuwa 80% ya wasanii wanaochezwa si wa pwani. 
5.MZIKI MZUKA YA BARAKA FM
Japokuwa Baraka fm ndiyo stesheni iliyoanza zamani sana pwani, imeshindwa kumiliki na kutawala kwa show za kuwakilisha mziki wa pwani. Mziki mzuka show inayoongozwa na aliyeshinda tuzo la mtangazaji bora wa kiume kwa coast awards 2013, Billy Miya kuanzia saa tatu hadi saba mchana husisimua na kuleta interviews za wasanii wanaoibuka na wanaopeta mkoani pwani.Vilevile mziki mzuka huwa na countdown yake kila mwisho wa wiki. 
4.MWAKEMWAKE YA PILIPILI FM.


Presenta Chigulu Ngala aka Chigz na the man with the bass Chris watachukua nafasi ya nne kwani drive show yao ni moto wa kuotea mbali. Chigulu ambaye ni mcheshi sana ana ufasaha mkubwa wa kuhoji wasanii na kuleta vipaji vipya kila uchao. Wasanii wa pwani hupewa kipao mbele na mada zinazosisimua hujadiliwa .Jumamosi mapresenter hao hushikana tena kuleta show moja ya kukata na shoka pale nyimbo za pwani hupambanishwa na za pande zingine za East Afrika kwenye top ten. 3.TAFRIJA SELECT YA PWANI FM. 
Bila shaka Arnold Munga katika watangazaji wote wanaokuza vipaji vya pwani yeye ndiye mlezi halisi. Munga ambaye pia ni mwanamuziki wa kundi la muziki wa gospel la The Mungaz hupeperusha kipindi hiki kuanzia saa kumi hadi mbili usiku jumatatu hadi ijumaa.Wasanii wa pwani hupewa nafasi ya mbele kabisa na nyimbo mpya kuchambuliwa moja baada ya nyingine. Kila Ijumaa nyimbo mpya hutambulishwa.Vilevile kipindi hiki hupendwa na wengi kwa jinsi mtangazaji Munga huleta ucheshi kwenye hadithi na stori zake za mitaani.
2. MASHAVMASHAV UNIRVESITY PWANI FM. 


Bila shaka toka enzi za Donde Samora aliyeanzisha kipindi hiki pwani fm hadi Gates aliporithishwa, MMU imekua mstari wa mbele kuwakilisha mziki wa pwani. Presenta Gates ambaye ameleta pamoja talanta tofauti na kuziweka pamoja ili kuendesha kipindi ana wafuasi na mashabiki wengi mno. Wasanii wengi wamejenga jina na fanbase zao kupitia mashavmashav, tamasha za muziki na interview za kukata na shoka pia wamepata. Kando na hayo Gates amewapa wasanii wa hiphop nafasi ya kujionyesha na kujitambulisha kwa jamii kupitia hiphop cypher thursday. Kila ijumaa kipindi hiki huwa na countdown moja bab kubwa na kwa kweli MMU wanapaswa kupewa hongera. 1.KAYA FLAVAZ RADIO KAYA. 

 Itakuwa bayana kuweka show hii nafasi ya kwanza kwani haina hata upinzani. Kaya flavaz inayoshikanishwa kabisa na chipkizi za kaya imelea vipaji vya wasanii wa pwani vilivyo. Kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa tatu asubuhi hadi saba mchana kila sehemu ya pwani maskio huwa kwa kipindi hiki. Chini ya mtangazaji Sister Shanniez na mwelekezi wake Teddy Nyae wa Tinga mashabiki wa muziki wa kizazi kipya pwani hupewa wanachokihitaji. Interview motomoto na mijadala ya sanaa ya pwani hujadiliwa.Jumapili usiku sis shaniz hupeperusha kali zetu, nyimbo kumi bora mkoani pwani na saa nne hadi sita usiku wasanii wanaoibuka ambao hawajawahi sikika kamwe hupewa nafasi kwa kuchezeshwa nyimbo zao hewani na kutambulishwa kwa jamii. Jambo linalofanya kipindi hiki kuwa original kabisa ni kuwa kinasikizwa na mashabiki wa umri mkubwa kwa mdogo,vijijini hadi mijini wote huskiza kipindi ikilinganishwa na vipindi vingine vinavyokuza mziki wa pwani.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA