SANAA YA PWANI: WANAOJISIFU NI WENGI WENYE MAPATO WACHACHE.
Karibuni kwenye sanaa ya pwani mwa Kenya mahali ambapo wanaojua muziki ni wengi kuliko mashabiki (anayepinga aseme). Mahali ambapo kila mtaa una studio yake ambazo nyingi zatoa mziki poor quality. Mahali ambapo wasanii hawapendi au hata hawalipi studio fee kabisa na hupenda vya bure kabisa. Mahali ambapo wasanii wengi hawajui wanalolifanya na wakikosolewa hukasirika na kuanza kutukanana hadharani.
Mahali ambapo msanii hujulikana kama supastar kwenye kituo kimoja cha redio na kamwe hajulikani kwenye vituo vingine vilivyo karibu. Mahali ambapo mapresenters huchukua hongo ili kucheza muziki. Mahali ambapo wasanii chipukizi huitisha pesa ili kushirikiana na chipukizi wenzao. Mahali ambapo....(wacha nisimamie hapa kabla sijawakasirisha wengi zaidi).
Kuna wanaojivunia mapato ya muziki na jasho lao,kwa mfano dada yetu msanii Nyota Ndogo. Yeye pekee ndiye aliyejenga nyumba kupitia mapato ya muziki.Wengine wameanza muziki jana washaanza kujisifu. Mara wengine wameacha.Muulizeni Nyota ndogo alianza lini na amepitia magumu yapi mpaka ajenge nyumba. Kazeni buti na muache lawama nyingi.
Kuchezwa redioni hakumaanishi wewe ni Superstar. Wangapi wamechezwa na bado wanalala kwa nyumba za kukodi,kutembea kwa miguu na hata kukopa produza ili wafanyiwe muziki bure? Ni hayo tu. Mwenye malalamishi aendelee kulalamika.
Comments
Post a Comment