REFIGAH ASAFISHA JINA LA GRANDPA NA KUMPA MOTISHA KIGOTO.


 Siku ya Jumapili tarehe 20 nilipata fursa ya kumhoji Refigah aliyekuwa amepitia Mama ngina Grounds kwa tamasha la Coast All Artistes Fiesta. Hii ni pale baada ya baadhi ya wasanii wa pwani kukashifu studio za Nairobi hasa Grandpa recordz kuwasajili wasanii wa pwani na kuwatumia bila wao kupata mapato yoyote.
Refigah hakutaka kuficha lolote bali alikuja wazi na kusema kuwa kabla msanii aanze kufanya kazi Grandpa recordz, yeye hupatiwa mkataba ausome mwanzo kisha akijiskia kwamba yupo katika uelewano na huo mkataba ndipo anaposajiliwa.
"Wasanii wanaposajiliwa na kufanywa wawe masupastar wanajisahau pindi tu wanaposhika pesa na kupata umaarufu. Wengi wao wanazitumia pesa zao ovyo na wanapoishiwa wanaanza kulaumu Grandpa recordz.Kama kuna msanii aliyenyanyaswa pesa zake au haki yake ana uhuru wa kwenda kortini kushtaki.Wafuate sheria si mambo na kuongea ovyo ovyo tu...."Alisema Refigah.
 Vilevile nilipata fursa ya kumuuliza Refigah kama anamfahamu Kigoto Mmbonde. Alijibu hivi,"Kigoto simjui wala sijawahi kumuona wala kumsikia ila kama kweli ana kipaji na anataka kujiunga na serikali ya Grandpa basi milango i wazi,aje atuonyeshe kama anao uwezo...." 
Kando na hayo,Refigah alisifu sana sanaa ya pwani na akaahidi kuja kufanya tamasha moja kubwa la talent search litakalo wapa wasanii wanaoibuka nafasi ya kusajiliwa kwenye studio za Grandpa Records.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA