DAZLAH BADO NDIYE COAST BEST LIVE PERFOMER



 Alipanda juu ya jukwaa na mashabiki wote wakapagawa na kurusha mikono hewani kwa vifijo na nderemo.Pindi tu aliposhuka stage nilipata nafasi ya kumhoji moja kwa moja jinsi anavyowapeleka mashabiki roho juu na kuwaacha wakiitisha zaidi.Mwanzo kama mjuavyo msanii Dazlah alishinda tuzo la best live perfomer kwa tuzo za coast music awardz 2013.Tulimuuliza hivi;Je ni siri gani unayotumia ili uwe perfomer mkali namna hio?
 "Mwanzo lazima upende unachokifanya na upige tizi kwa wingi,kwa hivyo mimi hupenda sana kudance,kutumbuiza watu na vilevile hupiga tizi ya kuperform stage kila mara ili niweze kuwa milele best live perfomer," alijibu Dazlah. Pia nilimuuliza msanìi huyu wa 'mlevi wa mapenzi' sababu ya yeye kunyoa dreadlocks zake na akajibu kuwa ni wakati wa kugeuza image yake kama msanii.Vilevile Dazlah alidokeza zaidi kuwa yupo na nyimbo mpya kabisa akimshirikisha Chikuzee na itaachiliwa hivi karibuni.Kwa sasa wimbo wake Bangereba umeshika chati za muziki wa pwani.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA