Posts

Showing posts with the label Music

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA

Image
Mwanamuziki tokea pwani ya Kenya,P-day ametoa kauli yake kuhusiana na matukio ya mauaji ya wazee wanaoshukiwa kuwa wachawi pande za Kilifi. Msanii huyo aliyetamba kwa kibao tarumbeta,Nylon guitar,Visingizo,Niringe naye na vinginevyo amedokeza haya kupitia ukurasa wake wa facebook akikashifu vikali vitendo hivyo. P-day alisema ya kwamba usemi wake anaopenda kuusema kwa nyimbo zake....."MZEE HATEMEWI MATE" unapaswa kuwa kauli mbiu itakayochukuliwa na kuwekwa kama mtajo utakaowaokao wazee kutoka kwenye janga hili. Tukinukuu kutoka alichonakili kwenye akaunti yake ya facebook..... "Social cohesion department to buy the mzee hatemewi mate lebol ( uzee si uchawi ) nliamka tu nkatunga hii lebol din't know itafika huku ........Sasa vijana kilifi county walianza kuua wazee kwa kua niwachawi BT sio Kila mwenye mvi ni mchawi ..let's respect the old" JE MAONI YAKO NI YAPI KUHUSIANA NA PENDEKEZO LA P-DAY KUHUSIANA NA WAZEE KUUAWA?

FAHAMU MSANII WAKO : MAHOJIANO NA MSANII HARUN DEEY

Image
FAHAMU MSANII WAKO : MAHOJIANO NA MSANII HARUN DEEY PWANI USANII:HARUN DEEY NI NANI HASWA? HARUN : Harun Iddy almaarufu Harun Deey alizaliwa 22/02/1997 na nilianza muziki alnikiwa na umri wa miaka kumi na sita. PWANI USANII:NYIMBO YAKO YA KWANZA ILIKUA GANI? HARUN: NASUBIRI ndiyo iliyokuwa nyimbo yangu ya kwanza ikifuatiziwa na NYOTA, zote nilizifanya Liwazo records,Mombasa. PWANI USANII:LABDA ULIANZA KUPATA UFANISI LINI KWENYE TASNIA YA MUZIKI? HARUN: Nilianza kupata ufanisi kupitia kwa wimbo wangu wa tatu unaojulikana kama BOSS DON ulioniwezesha kupata show kwenye vilabu tofauti vikiwemo HYPNOTICA (VIPAJI NIGHT), Z LOUNGE (XTRAVANGANZA NIGHT) na DANS LOUNGE (CELEBRITY THURSDAYS). Vilevile siwezi upuuzia wimbo wangu unaojulikana kama MAJARIBU manake ndio ulionipatia video yangu ya kwanza. PWANI USANII:JE VIDEO YA MAJARIBU ILIFANYA VYEMA AMA? HARUN: Ndio ilifanya vyema,iliweza kuchezwa kwenye Y254'S PWANI SHOW,Y IN THE MORNING,KBC na RAIA TV. PWANI USANII:NYIMBO...

MSANII MKUBWA WA PWANI AGEUKA KUWA MGANGA HATARI!!!!!!

Image
Ni habari motomoto na za kutamausha zilizofikia meza yetu ya habari hivi majuzi. Msanii chipukizi anayetokea mtaa wa Mbandi,gatuzi dogo la Kinango amewashangaza wengi pale alipoupiga teke usanii wake kwa muda na kujiunga na uganga. Msanii huyo chipikuzi anayejulikana na wengi kama Boss Michapo amekua mganga sifika guku akivutia wateja wengi kutoka kanda yote ya pwani. Michapo amekua akivuma kwa vibao motomoto vinavyopigwa sana kwenye madisko vumbi na disko matanga. Ilifikia wakati msanii huyo alipogonjeka na kwenda nchi jirani ya Tanzania kutibiwa ndipo aliporudi na kuwa mganga hodari. Inakisiwa kuwa Boss Michapo alienda Bongo na kununua mkoba wa uganga. Hivi sasa msanii huyu huenda studio na kulipia wasanii wenzake wamuandikie nyimbo kwa sababu hana muda wa kukaa chini na kuandika nyimbo. Jamaa huyu vilevile amesema hivi karibuni atasifika Afrika Mashariki yote kwa kuwa amepanga vibao motomoto na atatumia nguvu zake za kiganga kupenya kwenye soko la muziki. Vilevile amewakaribishw...

MSANII SHEPHARD KAMFANYA NINI PROMOTER WAKE LUKESMART ?

Image
BAADA YA PURUKUSHANI ,JE MSANII SHEPHARD KARUDIANA NA PROMOTER WAKE LUKESMART ENTERTAINMENT???? Ni mnamo mwezi wa saba pale vute nikuvute zilitanda kati ya msanii Shephard na promota wake Lukesmart. Baada ya Lukesmart kumsimamia Shephard kwenye project zake kadhaa na kuandaa tamasha nyingi wawili hao walianza purukushani na malumbano hadi ikapelekea uhusiano wao wa kikazi kuvunjika. Ni hivi majuzi tu baada ya Shephard kutoka safari zake za Zanzibar na Tanga ambapo Shephard alipost picha akiwa na promoter wake wa zamani Lukesmart. Vilevile si muda mrefu tayari Shephard akadondosha kibao kipya akimshirikisha Dazlah kwa jina 'CHEKO'. Tazama hapa - >https://youtu.be/O-Tdf6XmCSU

MASAUTI APAZA SAUTI ZAIDI GAGA

Image
MASAUTI APAZA SAUTI ZAIDI Ali Mohamed Said,almaarufu Masauti amepaza sauti kwa mara nyingine tena. Msanii huyu aliyetamba kwa vibao kadha wa kadha vikiwemo Mahabuba,Nurulain na vinginevyo alitudokezea kuhusu kazi yake mpya Gaga. Wimbo huo unaozungumzia tamaa ya kumtongoza binti mwenye hadhi ya juu umeyaleta mawazo yake msanii huyu aliyeandaa wimbo wake chini ya producer Motiff. "Video ya wimbo Gaga ipo tayari na iliandaliwa Mombasa na vilevile Nairobi,hivi karibuni itawachiliwa rasmi." Alitudokezea Masauti. Kupitia meza yetu ya habari,msanii huyu yupo katika safari ya kuiteka Afrika Mashariki kwa vibao motomoto alivyovitayarisha na atavidondosha tu pindi wakati murwa utimiapo. Kwa sasa tazama video yake ya awali....NURULAIN --- > https://youtu.be/8gIsxa3uEYA

SIJAWACHA MUZIKI BAADA YA HARUSI MSANII SHEPHARD APASUA MBARIKA

Image
SIJAWACHA MUZIKI BAADA YA HARUSI,MSANII SHEPHARD APASUA MBARIKA. Msanii Shephard amevunja ukimya wake baada ya kufunga harusi na kwenda chini ya maji. Shephard wa kibao kikali cha 'mdogo mdogo' kupitia mahojiano ya njia ya simu amedokezea meza yetu ya habari kwamba baada ya harusi alienda fungate (honeymoon) na mkewe kama inavyotakiwa. Msanii huyu aliongezea kuwa kwa sasa ameshajitayarisha kimuziki na tayari yupo na kibao kipya kwa jina 'cheko'. Kibao hiki amekitayarisha chini ya produza Tee wa Tee Hits productions. Video yake imefanywa na Director Nezzoh Monts na punde si punde atawachilia mzigo. Kaa mkao wa kula,usicheze mbali !!!

KELECHI ADONDOSHA VIDEO MPYA 'WATAISOMA NAMBA'

Image
KELECHI ADONDOSHA VIDEO MPYA 'WATAISOMA NAMBA' Msanii produza Kelechi Afrikana amejibwaga tena ulingoni. Msanii huyu aliyechini ya kubwa studios ameangusha kichupa chake kipya kabisa alichomsihirikisha Dj 2one2 . Msanii huyu mwenye sauti nzito yakuvutia na kunasa hisia amekua akitoa hit after hit na zinapokelewa vyema. Video hii imeandaliwa na Director Ricky Bekko na usafi wa picha na mnaso wa rangi umeipamba vyema video hii. Mandhari ya kuvutia na uhalisia wa hali ya juu umetumika. Tusiandike kwa mate ilhali wino upo jitazamie mwenyewe hapa --- > https://youtu.be/nxeBev6C_8w https://youtu.be/nxeBev6C_8w

CLD ARUDI KWA VIDEO MPYA ALIYOSHIRIKISHWA

Image
https://youtu.be/Dcm23CN9_7U

PRODUZA AMZ ATAMBULISHA KAZI YAKE YA KWANZA 2018.

Image
Produza shupavu tokea pwani,Amz wa Tempoz records ametambulisha kazi yake mpya kabisa mwaka huu. Huku akimregesha msanii aliyekuwa amekimya kimuziki,Cld. Icheki hapa -- > Wale wale D Rush Ft. CLD Lil Guy G Vid Produzza https://youtu.be/Dcm23CN9_7U

MWINYI KAZUNGU (TOP MASHARIKI) AMSIFIA DULLY MELODY KWENYE INTERVIEW MPYA!!!

Image
MWINYI KAZUNGU (TOP MASHARIKI) AMSIFIA DULLY MELODY KWENYE INTERVIEW MPYA!!! Mtangazaji sifika Afrika Mashariki, Mwinyi 'Mtetezi' Kazungu wikendi iliyopita alidunda Pwani kwa kuandaa show kadhaa za kipindi chake cha Top Mashariki TV show kwa KBC. Mtetezi, katika pilka pilka zake alipata fursa ya kumhoji msanii Dully Melody katika maeneo ya Pirates beach na hapo ndipo aliposhuhudia kipaji cha mkali huyu kutoka Pwani. "Kusema kweli, Dully Melody ni mwenye kipaji si haba.Ni mara yangu ya kwanza kumfanyia interview na nimeona kipaji chake kitanawiri na mimi binafsi pia nitahakikisha dau Lake la sanaa laelea Juu. Nimekuza vipaji vingi vya Pwani na Dully bila shaka amenionyesha anao uwezo."Alidokeza Mtetezi. Presenta huyu ambaye yupo mstari wa mbele kwa kuenua vipaji vipya si Pwani pekee bali Kenya nzima aliongeza kwamba atarudi Pwani kuja kufanya show zaidi za kipindi chake cha Top Mashariki kwani huku ndiko kwenye chimbuko halisi la vipaji vinavyoibukia. Kwa mengi...

ONE ON ONE WITH RICKY BEKKO.ONE OF THE BEST VIDEO DIRECTOR IN KENYA.EXCLUSIVE INTERVIEW!!!!

Image
LIGHTS, CAMERA, ACTION!!!! JUST SIX QUESTIONS FOR RICKY BEKKO. 1.What's your government names? RICKY :My government names are Ricky Bekko but a lot people think its an industry name not unless they send Mpesa or do any formal business that require signing of documents. 2.Did you ever dream of being a video Director/producer? RICKY :Actually, not growing up i never knew what i want to be but i would have been a lawyer if I had the chance to go to campus but our family wasn't well off. So in the process of hanging out with my friends who were musicians and seeing their struggle of shooting videos thats how i slowly ventured into this industry. 3.Which schools did you attend? RICKY:I went to Mariakani primary school and did my kcse in Good Samaritan High school in Kawangware that was it. The rest was what i call school of had knocks thats where you learn to survive through each means. I used to sell water, simcards, i was once a waiter in a local hotel and mo...

DOGO RICHIE ANIHARIBIA BIASHARA KWA KUTONGOZA WASANII WA KIKE WAKIJA STUDIO--PRODUZA AMZ ATOBOA SIRI!

Image
DOGO RICHIE ANIHARIBIA BIASHARA KWA KUTONGOZA WASANII WA KIKE WAKIJA STUDIO--PRODUZA AMZ ATOBOA SIRI!!! Idadi ya wasanii wa kike ndani ya studio za Tempoz imepungua sana jambo lililomfanya Produza Ammz kuongea. Jambo hili limeleta ugonganishi kati ya studio ya Tempoz na msanii Dogo Richie kwani yasemekana kuwa msanii huyu ana tabia ya kuwatongoza wasanii wa kike pindi wanapokuja studio. Dogo Richie kwa sasa, kama tulivyobaini ametongoza zaidi ya wasanii sita wa kike na kuwadanganya kuwa atapiga nao kolabo na kuwashika mkono kimuziki ili waweze kujulikana kwa urahisi. Jambo hili ndilo lililomkera produza Amz ambaye vilevile ni mmiliki wa studio hiyo. Amz alisema ya kuwa jambo kama hilo linamuharibia biashara na hadhi yake kama produza. "Wasanii wote wa kike wameacha kuja studio na pia idadi ya customers wangu wa kike pia imepungua tangu Dogo Richie akinyage studio. Tabia kama hizi ndogo ndogo ndizo zinazokandamiza sanaa ya Pwani na kupoteza vipaji vya mabinti bure. Nimejaribu...

UKINIJIBU NAKUROGA - - - KAULI YA SUSUMILA KWENYE WIMBO WAKE MPYA TEBWERE download it here!!!

Image
Msanii mkali tokea Pwani, Susumila amezuka tena na disstrack kali sana. Susumila baada ya kutajwa na msanii Dogo Richie kwenye nyimbo ya majanga, msanii huyu wa Tuliza Nyavu ameachia kibao chake huku akitoa misemo mikali... "Majanga ni msanii kuishi nyumba ya tenga mbili....." Akiongeza msumari Moto kwenye kidonda jamaa huyu wa Wachawi international alimalizia kwa mistari kuwa msanii yeyote atakayejibu diss hii yake atamroga. Haya nani yuataka kurogwa!!???? Ipakue nyimbo yenyewe hapa >> http://mdundo.com/song/97049

MSWAZI MASAUTI KUMBE KASAJILIWA NAIROBI TENA!!!!!

Image
MSWAZI MASAUTI KUMBE KASAJILIWA NAIROBI TENA!!!!! Msanii wa miondoko ya swahili RnB Mswazi Masauti amezuka tena baada ya kimya Kirefu. Meza yetu ya habari imebaini kuwa jamaa huyu baada ya kuwachana na Lebo ya Swarnb alipokuwa amesajiliwa chini Ya produza Ted Josiah, Mswazi amesajiliwa chini ya studio zilizoko Nairobi. Kwa mara nyingine tena,msanii huyu wa kibao cha 'Mahabuba' ameweka guu lake ndani ya jiji kuu la Nairobi na kupata fursa ya kufanya kazi chini Ya usajili wa Melwood studio ambapo atafanya kazi Na produza anayebobea, Motiff. Produza huyu amefanya kazi na wasanii kama Khaligraph Jones, The Kansoul na wengineo. Baada ya mawasiliano na msanii huyu, Masauti alidokeza kuwa kuna ngoma nyingi tu ambazo amefanya na hivi karibuni zitawachiliwa rasmi.

KILA MTU NA MSIMAMO WAKE NDIO SANAA INAVYOENDA ASEMA PRODUZA AMMZ

Image
KILA MTU NA MSIMAMO WAKE NDIO SANAA INAVYOENDA ASEMA PRODUZA AMMZ Produza na mmiliki wa studio za Tempoz, produza Ammz Jadidi au Tone la Maji ametoa kauli yake kuhusiana na maoni yatolewayo kuhusu sanaa. Haya yote yanajiri baada ya maswala kadha wa kadha kuibuka, yakiwemo show ya msanii Tekno Miles iliyobuma na Anita Santuri wa Pwani Celebrity Awards kusuta Cartels za muziki wa Pwani. Ammz amekuwa muwazi sana na kusema kuwa kila mmoja huwa na msimamo wake dhabiti anaouamini. Pasi kupoteza muda Soma alichonakili produza huyo hapa.... "Nimekuja kugundua hapa Kenya usiwahi kubishana na mwenzako kuhusu sanaa ya mziki inavyopaswa kuendeshwa. Kwa sababu kila mtu anajua na anaamini kila "point" anayoitoa. Washikadau wako na misimamo mikali wanayoiamini pa kubwa sana. Tatizo ni kuwa misimamo hii inatofautiana kutoka kwa mshikadau mmoja hadi mwengine. Na endapo utalazimisha kubadili msimamo wa mtu basi huenda ukajijengea chuki na huenda ukaharibu hata kazi yako. Hali hii i...

ANITA WA PWANI CELEBRITY AWARDS AGADHABISHWA NA CARTELS ZA MUZIKI PWANI!!!!!

Image
Anita Santuri, ambaye wengi wetu twamfahamu kupitia tuzo za Pwani Celebrity Awards na Ashantyz promotions amegadhabishwa sana na tabia ya washika dau wa sekta ya muziki pwani. Mwanadada huyu ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha Mseto East Afrika cha Citizen TV aliyatoa maneno haya tarehe 9,mwezi wa Septemba huku akilalamika sana kuwa wasanii wanaoibukia hawapewi nafasi kwa sababu jamaa wamejenge Vikundi vya kivyao vyao ili wajipe support wao kwa wao. Anita alipachika haya kwenye Facebook.... "I'm so disappointed at some of the coast entertainment stakeholders. .... why not support? ?? why not give chances to talents?? why create a crew that is enclosed not allowing change? ?? is it coz you think the other person will outshine you? but that's how you create healthy competition yawa..... then unakaa kwa TV ukisema vile umesaidia watu wengi!!!!! really !!!!!!! anyways tushawazoea. bora uzima hata nyerere na moi walikua raisi hivi wamestaafu..... UTASTAAFU PIA. ........

RAPPER WA KIKE TOKEA PWANI AWACHIA PINI JIPYA!!!

Image
RAPPER WA KIKE TOKEA PWANI AWACHIA PINI JIPYA!!! Idadi ya wasanii ikizidi shuka hasa hapa Pwani, msanii wa kike anayetamba kwa mtindo wa hiphop, Boomer Best amekuja vikali kwa video mpya. Boomer Best aliye chini Ya Young Boss music alipiga wimbo hatari kwa jina 'Mtoto wa Kike' na video kufanywa na Director Lamar. Video hiyo yapatikana kwenye you tube. Icheki hapa.... ameweza? https://youtu.be/ZPKx9vZBXmo

SIRI YA MSANII HUYU KUANDAA VIDEO YAKE NDANI YA NYUMBA YA TYCOON FLANI WA KENYA YAFICHUKA!!!!

Image
SIRI YA MSANII HUYU KUANDAA VIDEO YAKE NDANI YA NYUMBA YA TYCOON FLANI WA KENYA YAFICHUKA!!!! Pilka pilka zikizidi pamba moto kisiasa, wasanii wa Kenya wameamua kutosubiri moto huu kuzima. Jambo hili ndilo lililomfanya msanii anayeibukia vizuri kutoka Kenya, Beka the Boy kuingia ndani ya nyumba ya mchoraji sifika duniani Giampaolo Tommasi ili aweze kutengeneza video yake. Hivi je kusudio lake kuu lilikua lipi? Meza yetu ya habari ilibaini kuwa msanii huyu alitaka kupata picha na mvuto wa tamaduni tatu tofauti zikiwemo Swahili, Giriama na Italiano. Nyumba ya jamaa huyo, Giampaolo Tommasi imepambwa kwa picha za kuvutia zinazoleta tamaduni zote tatu pamoja hivyo basi mshikamano na maana fiche zimebebwa vyema kabisa kwenye mandhari haya. Je video ya wimbo wenyewe ni ipi? Ni swali wanalojiuliza wengi wa mashabiki. Tukizipunguza dukuduku zenu, wimbo wenyewe wajulikana kama "Jidai" uliotayarishwa na produza Totti La Inter na video imetayarishwa na produza anayebobea sana kw...

JE JAFFARIZOH KAWACHA MUZIKI NA KUWA VIDEO DIRECTOR??? PATA UKWELI HAPA!

Image
JE JAFFARIZOH KAWACHA MUZIKI NA KUWA VIDEO DIRECTOR??? PATA UKWELI HAPA! Huku akibandika picha hizo kwenye kurasa zake za Facebook, Ryzo huandika na kupiga Lebo picha zake kwamba kampuni yake ya video ni ANOTHER LEVEL FILMS. Ni majuzi tu pale alipobandika picha na kudai kuwa ana wimbo mpya ulioandaliwa na produza Morbiz na video chini Ya kampuni yake ya Another Level Films. Huku akibandika picha hizo kwenye kurasa zake za Facebook, Ryzo huandika na kupiga Lebo picha zake kwamba kampuni yake ya video ni ANOTHER LEVEL FILMS. Ni majuzi tu pale alipobandika picha na kudai kuwa ana wimbo mpya ulioandaliwa na produza Morbiz na video chini Ya kampuni yake ya Another Level Films.