SHAMANIZ CONTRACT SAGA: PRODUZA KHALID ASEMA MAISHA YAKE YAPO HATARINI.
Tukinukuu kutoka kwa ukurasa wake wa facebook "NAHISI MAISHA YANGU YAPO HATARINI. Jana asubuhi kama nilivyosema, nilienda kwa lawyer nikafungua file kuhusu mzozo uliopo baina ya Shamaniz na A Million Records. kisha lawyer akaandika barua mbili, moja kwa shamaniz kumkumbusha kuwa ana mkataba na hafai kuuvunja kiholela, pili ikawa ya producer Totti kumjulisha kuwa kuna mzozo unao endelea kwa hivyo hapaswi kuachilia huo wimbo waliorekodi shamaniz na chikuzee mpaka waniandikie barua rasmi na kunijulisha ni asilimia ngapi Shamaniz na mimi tutapata endapo nyimbo hiyo itachezwa kwa radio na tv na hata pia downloads. Leo mwendo wa saa saba na dakika 25,nilipata simu kutoka kwa Musa Babaz.
Nikimnukuu haya ndiyo aliyosema.kadri akiongea langu lilikuwa kumwambia "endelea nakuskiza" wala sijajibishana naye. Alisema hivi..........."Wacha nikueleze kitu kimoja,i le process unaendelea nayo, endelea tu na hiyo process tuone nani atafikisha mwengine kwa ukuta. Fanya unavyojua nami mi nitafanya ninavyojua, wewe pita kulia nami napita kushoto halafu tutakutana kwenye traffic lights halafu hapo ndipo tutaongea" Hayo ndiyo maneno ya Musa babaz.
Swali nije? Mimi nimepitia kulia nikafuata sheria,je yeye kushoto atafanya nini? Anasema fanya unavyojua nami nitafanya ninavyojua? Je hivi si vitisho? Labda leo nipate ajali,l abda watu wangu wanaeza sema hii ndiyo kushoto iliyotumika? Tayari nimemtumia lawyer wangu conversation yetu ya simu baada ya kutumiwa na safaricom kwa hatua za kisheria na ushahidi kamili wa madai yangu. Nimemtumia Gates pwani fm conversation hiyo pia na nitamsihi kesho aicheze hewani kila mtu aiskie ya kwamba maisha yangu yapo hatarini.
Jana Shamaniz aliamua tusahau yaliyopita na atarudi studio tufanye kazi. Nilikaribisha kwa mikono miwili.kufikia sasa nina wasiwasi sijui ni kipi kinachoendelea nyuma ya pazia kuhusu swala zima hili.Pia najiuliza je ilikuwa makosa kumsign shamaniz? Je wema wangu unaniponza? Je kuna makosa nikipigania haki yangu? Kwanini Musa babaz analazima na shamaniz au hata hiyo nyimbo waliyofanya na chiku,Hivi mombasa hakuna wasanii wengine kama shamaniz tayari amesainiwa? Au ana dhamira gani kwa kulazimisha mambo?
Comments
Post a Comment