MATAZAMO WA MWANAMGAMBO - Jinsi ya kuboresha mziki wako.
Fuatilia wapinzani/washindani.
Angalia kwa ukaribu wanachofanya wengine katika tasnia ama wanaofanya style sawia na yako. Hakuna malimu mzuri kushinda adui yako kimziki. Unapokataa kuskiza wenzako wanafanya nini unakodolea mcho tishio la kusalia nyuma wakati mtindo unapobadilika. Iwapo wapinzani wako ni watu uliowatangulia kimziki, hakikisha hudharau ushindani wao kwani mara nyingi wao ndio hua wananafasi kubwa ya kubadili game sabab wamekusoma kwa mda ile hali wewe huwatambui uwezo wao.
Professionalism:
Zingatia utaaluma. Mziki ni kazi na kama kazi zengine una sheria zake. Unapochukulia mziki na uzito na kufanya shughuli zake ukizingatia sheria ndogondogo za tasnia, basi una nafasi nzuri ya kuboresha nguvu za kazi zako. Utaaluma huu unafaa kuzingatiwa katika kila sekta inayohusiana na mziki wako; kutoka kwa jinsi unavyofanya kazi na ma’producer,mashabiki hadi watangazaji na vituo vya redio. Inasikitisha kuona msanii anashindwa ku keep time hata kwa interview yake.AM msanii kavaa nguo za kusikitisha anapotembelea ofisi mbalimbali zinazohusu mziki wake. kuna nguo za kuvaa unapo fanya video na kuna nguo za kukutana na wakuu wamakampuni . professionalism inajenga heshima na utaona urahisi wakufanya kazi na watu wakubwa katika tasnia wenzako wakiona ugumu.
Mazoezi.
wazungu walisema “practice makes perfect”. usiwahichoka kurudia mziki hadi upate the perfect sound. rekodi hata nyimbo mia kabla ya kutoa wimbo mmoja kama unauwezo, ili uhakikisha kazi unayotoa ni ya uhakika. Wengi wetu huwa na haraka kumaliza kazi ichezwe maredioni ndio maana nyingi hazina maisha marefu katika tasnia. mzoezi pia yanahusisha jinsi ya kutumbuiza(performance) kuwa tayari kufanya show ya kukata na shoka kila unapopata nafasi ya kuperfom. iwapo unamazoezi hua unaurahisi wakufunika wenzako ambao hawajafanya zoezi la kuperfom mbele ye umati. hii inajenga heshima na kukuweka katika level tofauti na wapinzni wako.
Biashara.
Ipe safari yako ya kimziki mtazamo wa kibaishara. fanya mziki kama vile ungefanya biashara nyengine. Kazi unazowasilisha katika soko hakikisha zina revenue potential katika market. Jua soko linataka nini. haina haja kutayarisha ngoma ambayo utasifiwa na rafiki zako wa kariu na mashabiki wasiipende. tengeza wimbo amabo utapendwa na mashabiki hata kama mwarafiki zako wa karibu watauponda.acha mafans ndi wa ku guide.
Discipline.
Hapa nadhani sote tuanaelewa.
Comments
Post a Comment