NDANI YA KAYAFLAVAZ CHIKUZEE AMEUTAMBULISHA WIMBO 'MAPENZI NAYAJUA' ALIOMSHIRIKISHA CHEGE.
Wengi walijiuliza maswali mengi mno waliposikia kuwa Chikuzee amecollabo na msanii wa Bongo. Japokuwa haikuwa wazi ni msanii yupi aliyekuwa amemshirikisha wengi walitamani kujua ni nani aliyeimba na bingwa huyu wa kibebe,kichuna,penzi la wivu,mwacheni vilevile na nyinginezo.
Leo ilibainika wazi kuwa Chikuzee alimshirikisha Chege wa Bongo. Tunavyojua wazi ni kuwa Chikuzee alipenda sana mtindo na style anayoimba Chege.
Wengine pia walisema kuwa Chikuzee alimuiga Chege jinsi anavyoimba. Leo ndani ya kipindi cha Kayaflavaz kinachopeperushwa hewani na Sista shanniz ndani ya Radio Kaya, Chikuzee alitambulisha kibao 'mapenzi nayajua' alichomshirikisha Chege. Wimbo huo uliandaliwa ndani ya studio za Hornet recordz chini ya produza Tk2.
Comments
Post a Comment