BEEF SEASON 1:BEEF KALI ISIYOZUNGUMZIWA KATI YA KILIFORNIA VS LIKONAE



Kuna chuki na uhasama kuu wa kimuziki kati ya wasanii wanaotokea Kilifi na wale wanaotokea Likoni. Najua washika dau wengi wa sanaa ya pwani wanafahamu beef hii ila wameinyamazia kwa sababu zisizoeleweka. Mwanzo kabisa, beef hii imejengwa sana na studio mbili kuu ambazo ni Cracksound records ya Kilifi na Thundersound records ya Likoni. Cracksound records ipo chini ya uongozi wa produza Mfalme Jay Crak na nduguye Produza Lai huku Likoni's finest Thundersound records ipo chini ya Sherrif produza Morbiz. Kusema kweli pande zote mbili ni mizizi ya muziki wa pwani, tukiangalia Kilifi wasanii kama Susumila, Escobar, Mchafuzi wa Mapozi, Lai, Shaa biggy walikuwepo mziki wa pwani ulipokuwa bado mchanga. Likoni nayo inajivunia talanta mpwitompwito zilizoanza muziki wa pwani huku wengi wa mashabiki wakisema kwamba Likoni ndipo muziki wa pwani ulipoanzia. Manabii, Rudeboiz, Double-s aka Bwenyenye, Fat-S,Chikuzee, Watapishi na wengineo.
 Beef ya hood hizi mbili ilianza pale wasanii wa Likoni Longpitaz na Sudi Manjewa wanaofanya hardcore hiphop toka studio ya Thundersound walipomualika msanii Mchafuzy wa Mapozi wa studio ya Cracksound kufanya naye Collabo. Baada ya kutengeza wimbo tetesi zilijiri kuwa Mchafuzy alishindwa kuflow vizuri na mistari yake ilikuwa ya kitoto. Tetesi zingine zikaenea kuwa mchafuzy alipigia presenters tofauti wa redio ili kubania na kutofanya wimbo huo usichezwe hewani.



Kilichojiri ni matusi na kukashifiana kwenye mtandao wa Facebook na Longpitaz akatengeza disstrack akimshirikisha kakake. Disstrack hio kwa jina 'Uncle Kambuzi' ilitaja baadhi ya wasanii wanaotokea kilifi. Mchafuzy naye alinyamaza kimya mpaka hivi majuzi msanii anayetokea pande za Kilifi na yupo studio ya Cracksound alipopasua mbarika na kuwaeleza wasanii wa thundersound kwamba diss yao ipo jikoni na watakiona cha moto. 


Pande ya Thundersound nayo ikajibu kupitia kwa wimbo wa Sudi Manjewa mpya ambao kwa sasa upo kwenye chati ya redio kaya unao ongea kimafumbo kuhusu beef hio.

Tunachosubiri ni wakali wa Kilifi hasa wale wa Cracksound kama Mchafuzy mwenyewe, Masterkimbo the street major, Tupesh the kilifornia makaveli, LaiLai, Msanii Jaykah na wengineo watajibu pande ya Likoni Thundersound iliyo na kina Sudi Manjewa,Longpitaz na kakake,X-mathare,G5 kikosi na wengineo.

SHERIFF MORBIZ VS MFALME JAYCRAK OVER TO YOU!!

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA