ODINAREH AADHIMISHA MWAKA KWENYE GAME NA MATOKEO YA KURIDHISHA.
Kama alivyoandika kwa ukurasa wake wa facebook,hii leo alikua akiadhimisha mwaka mmoja kwenye industry ya mziki sio pwani tu ila kenya mzima.."I was Duncan,but Duncan was crucified on easter friday then on Easter Monday he ressurected as Odinareh Bingwa"..msanii huyu amefanikiwa kutimiza mambo mengi kimziki katika mwaka huo mmoja ikiwemo video yake ya kwanza kuchezwa str8up KTN,mziki wake kuchezwa ma redioni pwani na kenya mzima na ngoma kama money lover,Ghetto dreaming na Ipo siku ft kaa la moto,Track yake na Ohms Law Montana ya Make A Name iliongoza chati za pwani fm mwezi mzima na kuweza kuingiza mziki wake katika soko la itunes.
Rapper huyu pia aligusia kuwa tayari ana collabo mbili kali na wasanii wakali wa hiphop Nairobi ambao hakuwataja kwani alisema itakua 'surprise' kwa mashabiki wake mwaka huu.Rapper huyu ambaye amekua akipeperusha bendera la kelele records juu Anapangia kuachili album yake rasmi hapa nchini na Single mpya aliyoiperform Fiesta iitwayo PAPER .Kama isemavyo track yake Make A Name,Mwaka huo wake kweli amejenga jina kama mkali wa hiphop mombasani na msanii wa kutazamia nchini kenya
Comments
Post a Comment