PRODUZA JOHNIE BLAZE KUMBE MSANII PIA
Produza gwiji aliyekita mizizi kwa kazi zake zinazokubalika na wengi;Johnie Blaze leo hii amejitwika jukumu la kukata ukimya wake na kudondosha usemi kuhusu yeye na talanta ya kuimba.Wengi wetu tulikuwa hatujui kabisa kuwa Blaze ni msanii ila hii ilibainika wazi pale aliponakili kwa ukurasa wake wa facebook hivi......
"Nimeamua kutangaza rasmi,kando na kuwa producer wa muziki,sasa nitakuwa full time msanii kwa sababu kipaji ninacho!....." Meza yetu ya habari iliamua kumtafuta na kumhoji na Blaze alikuwa na haya ya kuongezea......."I am an artist,ni vile naconcentrate na production sana sina time yakufanya kazi zangu,but now ,its the right moment....." Najua sote tunayo hamu ya kusikiliza nyimbo zake produza Johnie Blaze.
Comments
Post a Comment