GANGSTAR APOLOGY: HAKUNA BEEF NI MUZIKI TU.
Miezi kadhaa iliyopita msanii Shiney na rapper Kassamoney walikuwa kwenye mgongano na kufikia hata Shiney kwenda polisi kumshtaki kassamoney. Mambo yalipozidi kupamba moto waliletwa pamoja na mtangazaji Gates wa pwani fm na kusameheana kwenye kipindi cha Mashavmashav.
Baada ya hapo lililofuatia ni Shiney kurekodi wimbo GANGSTAR APOLOGY akimshirikisha OHM'S LAW MONTANA ambaye ni rapper rafiki yake Kassamoney. Hili halikupokelewa vyema
na Kassamoney kwani fununu zajiri kuwa hakufurahishwa na collabo hio.
Wakati wa Mombasa Fiesta tulimsikia Ohm's Law akisema kuwa yeye alipigiwa simu na meneja wa studio ya bigfoot akafunike verse na akaipenda hio beat sana na kama mwanamuziki mwingine yeyote akafanya ipasavyo......
"Lengo langu lilikuwa kufanya mziki mzuri na binti Shiney, sijui kama Gangstar Apology ni diss au si diss......."Alisema Ohm's law.
Tulipowasiliana na Kassamoney,kwa upande wake hakuwa na mengi ya kunena bali alikubali kuwa ashawahi usikia wimbo huo na wote huo ni muziki.Kawaida ya muziki.
Comments
Post a Comment