Posts

Showing posts from April, 2014

WASANII WA KIKE WA PWANI WAZUNGUMZIA KUHUSU SHERIA MPYA YA NDOA NA KUOA.

Image
Ni Juzi tu Rais Uhuru alitia sahihi mswada wa kuoa bibi zaidi ya mmoja na leo wasanii wa kike wa pwani wamevunja mbarika na kuzungumzia jambo hilo. NYOTA NDOGO alikuwa na haya ya kunena..."sasa wanawake ndio watakao tafuta mpango wa kando kwa bidii.mume moja wake wanne?ukija kwangu umechoka kama nini hujiwezi.mume anaitaji mapumziko.haya akiwa na hawa wanne watapumzikaje?ndio kuridhisha wengine wengine kupata makombo yasio watosha.mpango wa kando." Naye SIS P hakusita kuöngeza chumvi na kunena hivi...."hehe ati polygamy is now legal in kenya.. mimi bwanangu akiongeza bibi mimi pia naongeza bwana na we be equal".Je wewe maoni yako ni yapi?

GROOVE AWARDS, NANI ALIYEPATA NOMINATIONS?

Image
PWANI SONG OF THE YEAR • Ahadi Za Bwana - Pst. Anthony Musembi • Bwana Wa Mabwana -Princess Farida • Milele - Marion Shako • Mwaminifu - Kristine Ndela Ft. Rozina • Nisamehe - Mercy D Lai • Tam Tam - Masha Mapenzi vile vile, Msanii Mecry D Lai aliweza kupata Nominations mbili kwenye Female Artiste of the Year na pia kwenye Album of The year, (Nisamehe)

WILBERFORCE WA HEARTBEAT ASHEREHEKEA BIRTHDAY YA MPENZIWE KWA NJIA SPECIAL!!!

Image
Promoter gwiji na muandalizi tamasha mashuhuri pwani, Wilberforce Mwikya wa Heartbeart entertainment leo hii ana furaha ya kukata na shoka pale anaposheherekea birthday ya bibi yake. Wilberforce aliweka picha ya binti huyu mzuri kwenye ukurasa wake wa facebook na kutangazia ulimwengu uzito wa penzi lake kwake.Wilberforce Jeff Mwikya Dah! .Binti huyo kwa jina Juliet Mkube hufanya kazi Coast Bus Mombasa office na yupo na miaka 23. Party ya sherehe hiyo ya birthday itafanyika Southcoast, Diani pale Jacaranda hotel. Vilevile promoter huyu amevunja ukimya wake na kutufahamisha kuwa amefungua pub kadhaa katika maeneo ya Majengo mapya Likoni, na punde atarudi kwenye ulingo wa uandalizi wa tamasha za burudani.

SHAMANIZ CONTRACT SAGA: PRODUZA KHALID ASEMA MAISHA YAKE YAPO HATARINI.

Image
 Tukinukuu kutoka kwa ukurasa wake wa facebook "NAHISI MAISHA YANGU YAPO HATARINI. Jana asubuhi kama nilivyosema, nilienda kwa lawyer nikafungua file kuhusu mzozo uliopo baina ya Shamaniz na A Million Records. kisha lawyer akaandika barua mbili, moja kwa shamaniz kumkumbusha kuwa ana mkataba na hafai kuuvunja kiholela, pili ikawa ya producer Totti kumjulisha kuwa kuna mzozo unao endelea kwa hivyo hapaswi kuachilia huo wimbo waliorekodi shamaniz na chikuzee mpaka waniandikie barua rasmi na kunijulisha ni asilimia ngapi Shamaniz na mimi tutapata endapo nyimbo hiyo itachezwa kwa radio na tv na hata pia downloads. Leo mwendo wa saa saba na dakika 25,nilipata simu kutoka kwa Musa Babaz. Nikimnukuu haya ndiyo aliyosema.kadri akiongea langu lilikuwa kumwambia "endelea nakuskiza" wala sijajibishana naye. Alisema hivi..........."Wacha nikueleze kitu kimoja,i le process unaendelea nayo, endelea tu na hiyo process tuone nani atafikisha mwengine kwa ukuta. Fany...

FISHERMAN : TUSAIDIE JAMII NA NAWAKARIBISHA JUMAPILI KWA EVENT YA TWAAYF CHILDREN CENTER .

Image
Mkali wa dancehall na ragga pwani na Afrika Mashariki kwa jumla, Fisherman amekuja wazi na kujitolea kutoa msaada wa BACK TO SCHOOL kwa watoto ya Twaayf orphanage. Fisherman aliyesajiliwa kwenye studio za Grandpa recordz ametueleza kuwa atakuwepo siku ya Jumapili ya tarehe nne ili aweze jumuika na watoto wanapojitayarisha kurudi shule.Vilevile msanii huyu anayevuma kwa kibao chizika akimshirikisha JO-1 amewakaribisha washika dau wa sanaa ya pwani na yeyote yule aliye na uwezo ajitokeze TWAAYF CHILDREN CENTER LIKONI ili aweze toa mchango wake wa BACK TO SCHOOL.

NDANI YA KAYAFLAVAZ CHIKUZEE AMEUTAMBULISHA WIMBO 'MAPENZI NAYAJUA' ALIOMSHIRIKISHA CHEGE.

Image
Wengi walijiuliza maswali mengi mno waliposikia kuwa Chikuzee amecollabo na msanii wa Bongo. Japokuwa haikuwa wazi ni msanii yupi aliyekuwa amemshirikisha wengi walitamani kujua ni nani aliyeimba na bingwa huyu wa kibebe,kichuna,penzi la wivu,mwacheni vilevile na nyinginezo.  Leo ilibainika wazi kuwa Chikuzee alimshirikisha Chege wa Bongo. Tunavyojua wazi ni kuwa Chikuzee alipenda sana mtindo na style anayoimba Chege. Wengine pia walisema kuwa Chikuzee alimuiga Chege jinsi anavyoimba. Leo ndani ya kipindi cha Kayaflavaz kinachopeperushwa hewani na Sista shanniz ndani ya Radio Kaya,  Chikuzee alitambulisha kibao 'mapenzi nayajua' alichomshirikisha Chege. Wimbo huo uliandaliwa ndani ya studio za Hornet recordz chini ya produza Tk2.

PRODUZA BAINDO & PRODUZA SULENAX WAIMBA NYIMBO JINA # WASIA

Image
Itashangaza wengi kwa maproduza gwiji wawili kuja pamoja kushirikiana kufanya kazi ya muziki hasa ya kuimba ilhali wengi wamewazoea kwa upande wa kuandaa beat na kuandaa muziki.  Raundi hii produza wa Bigfoot production Baindo na produza wa Liwazo recordz Sulenax wamekuja pamoja kutoa wimbo 'wasia' unaowapa advice wasanii wa pwani.  Katika wimbo huu,Baindo ameimba chorus huku sulenax akiwa kwenye verse akisaidiana na Baindo. Tulipowasilianana Baindo alikuwa na haya ya kunena "..... .imefikiapahali wasanii hawaaminiki tena wamekuwa wasaliti malumbano kila kukicha. Je wasanii wa pwani twasomeka vipi nje ya hii kanda ya pwani.? Sanaa ya pwani imekuwa kwa asilimia kubwa ila tunataka kuididimiza kwa asilimia kubwa zaidi hali hii ndio imenigusa mtima wangu kwa uchungu sana, je twaelekea wapi?   Tegeeni kibao baada ya juma moja.....

DAZLAH: SIKUAMBIWA NA MAMANGU NINYOE DREADS NA MIMI SI MSANII WA CANDY N CANDY

Image
Mkali wa miondoko ya muziki wa pwani, Kiduche almaarufu Dazlah amekuja wazi leo hii kuweka mambo wazi. Kwenye show ya mashavmashav alipohojiwa na presenta Eric Gates, msanii huyo alikana kuwa mamake mzazi ndiye aliyemwambia anyoe dread.  Uvumi ulikua eti Dazlah amemsahau Mungu na haendi tena msikitini ndiposa mamake akaingilia kati kwa hasira na kumwambia amrudie Mungu na anyoe dread aende msikitini kusali. Dazlah aliyapinga hayo na kudai ilikua hiari yake ya kugeuza image ndiposa akanyoa. Vilevile msanii huyu amevunja madai ya kuwa bado yupo candy n candy records. Dazlah alisema kuwa alitoka CandynCandy na hafanyi kazi tena na wao ila huwa anaweza shirikiana na wao kupitia makubaliano fulani."Naweza fanya kazi na CandynCandy ila hawajanisajili" alisema Dazlah.

Phyzo B, Born to Shine

Image
Phyzo B is a song writer,recording and performing Gospel artist. Phyzo is ready to deliver what the holyghost has sent him to give to the world. He started off his music career way back in high school down in Nairobi under Moon's entertainment but then he was doing secular music, not untill 2012 when the Grace of God fell upon him and had to turn from his past and change his ways. Phyzo B took one year off music completely till when he got an idea of his first gospel song 'BORN TO SHINE'.  This young lad listened to a hiphop beat and on it he just talked of God and his doings onto his life. So far he has three tracks 'MY SAKE'-Its all about the pain and suffering that Jesus went through for my sake.'POSITION'-Its­ a little bit a life teach song to all politicians that the position they are now its because of a common mwananchi that voted them so he has no reason to neglect anything the citizens ask from him or her.

SHAMANIZ CONTRACT SAGA:LIGHT AT THE END OF THE TUNNEL

Image
Baada ya mshike mshike,malumbano na mgogoro uliokumba A million Recordz na Shamaniz,mwangaza umeonekana na kweli siku njema imewadia.Jana pande zote mbili Shamaniz na A million recordz huku Rapdem akiwa shahidi zilikuja pamoja na kuelewana.Malumbano yakafikia kikomo.SHAMANIZ hivi sasa amerudi rasmi kimuziki na ataendelea kufanya kazi na produza Khalid.Twamtakia kila la kheri.

SANAA YA PWANI: WANAOJISIFU NI WENGI WENYE MAPATO WACHACHE.

Image
Karibuni kwenye sanaa ya pwani mwa Kenya mahali ambapo wanaojua muziki ni wengi kuliko mashabiki (anayepinga aseme). Mahali ambapo kila mtaa una studio yake ambazo nyingi zatoa mziki poor quality. Mahali ambapo wasanii hawapendi au hata hawalipi studio fee kabisa na hupenda vya bure kabisa. Mahali ambapo wasanii wengi hawajui wanalolifanya na wakikosolewa hukasirika na kuanza kutukanana hadharani.  Mahali ambapo msanii hujulikana kama supastar kwenye kituo kimoja cha redio na kamwe hajulikani kwenye vituo vingine vilivyo karibu. Mahali ambapo mapresenters huchukua hongo ili kucheza muziki. Mahali ambapo wasanii chipukizi huitisha pesa ili kushirikiana na chipukizi wenzao. Mahali ambapo....(wacha nisimamie hapa kabla sijawakasirisha wengi zaidi).  Kuna wanaojivunia mapato ya muziki na jasho lao,kwa mfano dada yetu msanii Nyota Ndogo. Yeye pekee ndiye aliyejenga nyumba kupitia mapato ya muziki.Wengine wameanza muziki jana washaanza kujisifu. Mara wengine wame...

SHAMANIZ AWACHA MUZIKI KWA MUDA HUKU DOGO RICHY NA LYPSO WAKIJIPA MOTISHA!!!

Image
Baada ya kuvuma na vibao motomoto na kufanya kazi na wasanii tofauti tofauti.Binti msanii niliyemsikia kwa mara ya kwanza kwa wimbo NIMEZAMA alikuja wazi hapo jana na kuongea hadharani kuwa ameupiga teke muziki. Shamaniz aliyevuma kwa kibao kama romeo and juliet na vinginevyo aliandika haya kwenye ukurasa wake wa facebook....."Nimekuwa nikiwaza sana na nimeamua kujipa likizo kiasi,yaani naacha kuimba kwa muda.nahitaji kuangalia maswala kadhaa ili niweze kujisimamia pasipo na kufanyiwa bure..to all producers whom i have worked with,presentersand my sweet fans thank u 4 ur time n support till we meet again love u all and God bless you...."  Imebainika wazi kuwa Shamaniz amewacha muziki kwa muda ili afanye maswala yatakayompatia hela za kulipia studio !! Huku Shamaniz akiongea hayo Lypso na Dogo Richy wanaobobea kwenye sanaa ya pwani na Kenya nzima kwa jumla walijitokeza na kunena haya kupitia kurasa zao za facebook....DOGO RICHY "I say wasanii kibao najua...

Ohms law Montana, Kendrick lamar's look alike

Image
Most of his fans say that he is Kendrick Lamar's look alike, do you agree?

NYOTA NDOGO COLLABO NA UKOO FLANI NDANI YA GRANDPA RECORDZ

Image
Magwiji wakuu wa muziki wa pwani ukipenda unaweza kuwaita coastal Kenya music legends Ukoo flani na Nyota Ndogo walikuja pamoja na kubadili mawazo. P.O.P ambaye ni mmoja wa kikosi cha hiphop Ukoo flani aliongea na Nyota Ndogo na wakaelewana kuwa watafanya kazi Grandpa Records. Nyota ndogo ndiye aliyetoa wazo hilo la ushirikiano mbele ya Refigah wa Grandpa. P.O.P naye aliunga mkono huku Refigah akiwakaribisha na kuwaambia wakiwa tayari waende Grandpa Records kufanya muziki. La kushangaza ni huo mtindo,style na beat za Grandpa,Ukoo Flani wataflow nazo kweli?

NO MORE MUSIC FAVOURS FROM DADDI Q!

Image
Mkali wa mtindo wa Dancehall na hiphop anayetokea Ukunda ila kwa sasa yupo jijini Nairobi anapofanyia muziki amekuja wazi na kusema yaliyomsibu. Daddi Q aliyetamba kwa vibao kama Nakuita,Tumerelax,Downtown Mombasani na vinginevyo alisema kuwa amechoka kusaidia wasanii kimuziki.Yaonekana sasa yuataka mambo ya nipe nikupe si mambo ya bure kama wasanii wengi wa pwani wanavyopenda.  Daddi Q alinakili haya kwenye ukurasa wa Facebook....."SINCE MY DAUGHTER WAS 3 TILL NOW SHE'S 10 YEARS I'VE BEEN HELPING PEOPLE RECORD FREE MUSIC TO FREE VIDEOS BUT NOW ITS ENOUGH PEOPLE HAVE USED ME FOR LONG, SOME HAVE USED MY IDEAS N CREATIVITY TO EARN FAME N CASH FROM TODAY I PUT A FULLSTOP NO MORE FAVOURS..NKT " Waliozoea vya bure habari ndio hio.

GANGSTAR APOLOGY: HAKUNA BEEF NI MUZIKI TU.

Image
Miezi kadhaa iliyopita msanii Shiney na rapper Kassamoney walikuwa kwenye mgongano na kufikia hata Shiney kwenda polisi kumshtaki kassamoney. Mambo yalipozidi kupamba moto waliletwa pamoja na mtangazaji Gates wa pwani fm na kusameheana kwenye kipindi cha Mashavmashav. Baada ya hapo lililofuatia ni Shiney kurekodi wimbo GANGSTAR APOLOGY akimshirikisha OHM'S LAW MONTANA ambaye ni rapper rafiki yake Kassamoney. Hili halikupokelewa vyema  na Kassamoney kwani fununu zajiri kuwa hakufurahishwa na collabo hio.  Wakati wa Mombasa Fiesta tulimsikia Ohm's Law akisema kuwa yeye alipigiwa simu na meneja wa studio ya bigfoot akafunike verse na akaipenda hio beat sana na kama mwanamuziki mwingine yeyote akafanya ipasavyo...... "Lengo langu lilikuwa kufanya mziki mzuri na binti Shiney, sijui kama Gangstar Apology ni diss au si diss. ......"Alisema Ohm's law.  Tulipowasiliana na Kassamoney,kwa upande wake hakuwa na mengi ya kunena bali alikubali kuwa a...

THE SECRET IS OUT!RAPDEM REVEALS 12 THINGS YOU DIDN'T KNOW ABOUT HER!

Image
1.Rapdem's favourite: Food ugali &Fish  2.Favourite book: Gifted Hands by Benson Carson  3.Rapdem doesn't take alcohol nor tea 4.Favourite Artiste Juacali  5.Napenda church sana hence very prayerful  6.Hobbies: travelling, reading and watching soccer  7.Favourite club: Manchester united  8.Like dressing anything as long as kimenifit  9.Whats in my handbag? My samsung phone, mirror, make ups, study book pen, tissues and watch. 10.Best quotes "tomorrow is always another day we get old."  11.Role model of course my mum  12.Rapdem is a perfoming artiste challenges makes her strong and healthy.

ODINAREH AADHIMISHA MWAKA KWENYE GAME NA MATOKEO YA KURIDHISHA.

Image
Kama alivyoandika kwa ukurasa wake wa facebook,hii leo alikua akiadhimisha mwaka mmoja kwenye industry ya mziki sio pwani tu ila kenya mzima.."I was Duncan,but Duncan was crucified on easter friday then on Easter Monday he ressurected as Odinareh Bingwa"..msanii huyu amefanikiwa kutimiza mambo mengi kimziki katika mwaka huo mmoja ikiwemo video yake ya kwanza kuchezwa str8up KTN,mziki wake kuchezwa ma redioni pwani na kenya mzima na ngoma kama money lover,Ghetto dreaming na Ipo siku ft kaa la moto,Track yake na Ohms Law Montana ya Make A Name iliongoza chati za pwani fm mwezi mzima na kuweza kuingiza mziki wake katika soko la itunes.  Rapper huyu pia aligusia kuwa tayari ana collabo mbili kali na wasanii wakali wa hiphop Nairobi ambao hakuwataja kwani alisema itakua 'surprise' kwa mashabiki wake mwaka huu.Rapper huyu ambaye amekua akipeperusha bendera la kelele records juu Anapangia kuachili album yake rasmi hapa nchini na Single mpya aliyoiperform Fie...

ERICK OMTERE THE 27 YEAR OLD VIRGIN/K24 ACTOR GETS SEX OFFERS FROM LADIES

Image
 Erick Omtere the top Kenyan actor from coast who feutures in K24 Tv series Almasi every sunday,monday and tuesday at 730 pm has been getting sex offers from various sexy ladies.and even some mama's have been stalking him.the actor's virginity has been the main topic on various kenyan blogs and Newspapers. The hunk actor who acts as jaffar in Almasi is set to fly to Nigeria soon for a movie shot.the actor has been stalked on his fb inbox and has been getting even alot of calls from unknown numbers.nway the actor is soon to open his films industry and build more other upcoming kenyan actors.Eric denied the sex offers and still maintains his principles of waiting for the right time to come

SHEMBWANA MASAUTI IS NOW A PROUD UNCLE

Image
They say, children are a gift from God and they are truly a blessing in our lives. Yembwana Masauti took to social media to reveal his excitement on being an uncle. Here are the pictures of his sister and the beautiful kid Congratulations!

part 2, fiesta photos

Image

Pictures of how the fiesta went down part 1

Image

Jokka Zunda The producer to watch out for

Image
Jokka Zunda ni producer ambaye anafanya vizuri katika maeneo ya pwani. Producer Jokka anatokea maeneo yakwa ndomo mjini Malindi city,pia vilevile ametengeneza filamu kwa jina mzunguko ambayo atailanchi hivi karibuni...Tegea uhondo...Terra Byte Rec ndio mpango mzima.

VIDEO YA VIVONCE ILIYOZUA UTATA KUMALIZIWA HIVI KARIBUNI.

Image
 Baada ya kuandaa video ya wimbo wake Yilele na kugonga mwamba katikati kwa tuhuma na vijimambo vidogovidogo visivyoeleweka.Binti mwenye urembo,umbo na sauti iliyokolea utamu Vivonce alikuja wazi na kutuvunjia mbarika kuwa producer wa video hiyo ambaye ni Hamza Omar wa One point One Montage atawasili Mombasa wiki hii kuendelea na uandalizi wa video hiyo.Vivonce aliongezea kuwa video hiyo itamaliziwa jijini Nairobi na mashabiki watarajie kazi nzuri itakayowaburudisha.

DAZLAH BADO NDIYE COAST BEST LIVE PERFOMER

Image
 Alipanda juu ya jukwaa na mashabiki wote wakapagawa na kurusha mikono hewani kwa vifijo na nderemo.Pindi tu aliposhuka stage nilipata nafasi ya kumhoji moja kwa moja jinsi anavyowapeleka mashabiki roho juu na kuwaacha wakiitisha zaidi.Mwanzo kama mjuavyo msanii Dazlah alishinda tuzo la best live perfomer kwa tuzo za coast music awardz 2013.Tulimuuliza hivi;Je ni siri gani unayotumia ili uwe perfomer mkali namna hio?  "Mwanzo lazima upende unachokifanya na upige tizi kwa wingi,kwa hivyo mimi hupenda sana kudance,kutumbuiza watu na vilevile hupiga tizi ya kuperform stage kila mara ili niweze kuwa milele best live perfomer," alijibu Dazlah. Pia nilimuuliza msanìi huyu wa 'mlevi wa mapenzi' sababu ya yeye kunyoa dreadlocks zake na akajibu kuwa ni wakati wa kugeuza image yake kama msanii.Vilevile Dazlah alidokeza zaidi kuwa yupo na nyimbo mpya kabisa akimshirikisha Chikuzee na itaachiliwa hivi karibuni.Kwa sasa wimbo wake Bangereba umeshika chati za ...

REFIGAH ASAFISHA JINA LA GRANDPA NA KUMPA MOTISHA KIGOTO.

Image
 Siku ya Jumapili tarehe 20 nilipata fursa ya kumhoji Refigah aliyekuwa amepitia Mama ngina Grounds kwa tamasha la Coast All Artistes Fiesta. Hii ni pale baada ya baadhi ya wasanii wa pwani kukashifu studio za Nairobi hasa Grandpa recordz kuwasajili wasanii wa pwani na kuwatumia bila wao kupata mapato yoyote. Refigah hakutaka kuficha lolote bali alikuja wazi na kusema kuwa kabla msanii aanze kufanya kazi Grandpa recordz, yeye hupatiwa mkataba ausome mwanzo kisha akijiskia kwamba yupo katika uelewano na huo mkataba ndipo anaposajiliwa. "Wasanii wanaposajiliwa na kufanywa wawe masupastar wanajisahau pindi tu wanaposhika pesa na kupata umaarufu. Wengi wao wanazitumia pesa zao ovyo na wanapoishiwa wanaanza kulaumu Grandpa recordz.Kama kuna msanii aliyenyanyaswa pesa zake au haki yake ana uhuru wa kwenda kortini kushtaki.Wafuate sheria si mambo na kuongea ovyo ovyo tu.... "Alisema Refigah.  Vilevile nilipata fursa ya kumuuliza Refigah kama anamfahamu Kigoto Mm...

MEET GORGEOUS JULIAN, ACTRESS FORM MALINDI

Image
she goes by the name Julian,talented actress and model from Malindi city.She has feature in Lost Ring Movie produced by Kabaka films which will be out soon.Her dreamz is to the next kenyan to win Oscar Awards

Meet BAKES aka MO BAKES

Image
BAKES aka MO BAKES real names Bakari Salim is a Kenyan born and raised poet, songwriter, singer, rap artist based in Nairobi, the Capital city of Kenya. Bakes is conversant with both oral and written English and Swahili language with an outstanding appeal of depth, vocabulary and versatility.  This talented rap artiste started recording late 2003 and in 2004 won SOS awards best composition and best HIP HOP song. Bakes took a hiatus from music to pursue his studies and late 2009 he decided to get back to music and did his first album THE NATHARIA.  The album was completed in 2011." The masterpiece talks about my experience and issues we face day in day out ," said Mo Bakes. Currently he has new singles as well as a duet album with one BLAQCHILD.  "I am a versatile artiste so my music varies across all major genres such as hiphop, r n b, blues, techno, dance,rap ,benga and bongo. I have so far written over 300 songs, personal as well as for others ,...

MAHABA YANOGA KWA EVE WA NZUMARI

Image
Eve Adhiambo ama ukipenda NZUMARI AWARDS C.E.O hapo jana kupitia ukurasa wake wa Facebook alitupia picha akiwa analiwa jate na jamaa wake mpya ambaye jina tumelieka kwenye mabano chungulia picha hio kwa makini ujue ni nani......  Na hivi ndio alisema kupitia Facebook “ Kwa mahaba unayo nipa nimenogewa…hakuna yule ashawai nionyesha mapenzi kama huyu mume wangu, amenigusa mahali sijawai kugswa, nampenda sana…haya wambea, wanablog na wenye uwivu habari ndo hio…..mimi na yeye milele, huyu ndo my baiby, my man, my hubby. ”-courtesy of THE GREAT MULLEY-

GHETTOSUPASTARZ:DJ BUNDUKI KEEPS SHOOTING HIGHER

Image
Ghettosupastarz entertainment started way back in 2004. This entertainment company has promoted lots of big artists in Mombasa, Nairobi and international artists as a well. Ghettosupastarz has big links with Jamaican artistes such as capleton, chris martin, richie loop, elephant man, aidonia, deniq ,ch­arly black,i wayne,I octane n many more. Not only that, this entertainment clique rules the streets with its mixxes. Dj Bunduki has more mixxes all over the streets in whole east africa than any other Dj. Ghettosupastaz plays all kind of music, from gospel,dancehall,hip hop,soul,house, trance,local,lingala,ragga riddims,oldskool, bongo and more.  They also train people how to mixx both video and audio songs at only 25,000ksh for 3months.Currently hype mix volume 34 and riddim doze vol 1 are now ruling the streets counrywide. This mixx promotes both local and international artists.Apart from that Ghettosupastarz currently plays live video mixxes alongside their you...

PRODUZA JOHNIE BLAZE KUMBE MSANII PIA

Image
Produza gwiji aliyekita mizizi kwa kazi zake zinazokubalika na wengi;Johnie Blaze leo hii amejitwika jukumu la kukata ukimya wake na kudondosha usemi kuhusu yeye na talanta ya kuimba.Wengi wetu tulikuwa hatujui kabisa kuwa Blaze ni msanii ila hii ilibainika wazi pale aliponakili kwa ukurasa wake wa facebook hivi...... "Nimeamua kutangaza rasmi,kando na kuwa producer wa muziki,sasa nitakuwa full time msanii kwa sababu kipaji ninacho!....." Meza yetu ya habari iliamua kumtafuta na kumhoji na Blaze alikuwa na haya ya kuongezea......."I am an artist,ni vile naconcentrate na production sana sina time yakufanya kazi zangu,but now ,its the right moment....." Najua sote tunayo hamu ya kusikiliza nyimbo zake produza Johnie Blaze.

KUTANA NA MR. MEDU

Image
Medu ni msanii aliyevuma sana kwa kibao kinachoitwa Nimeku kama chiz. Ni kibao kilicho mfahamisha kwa wengi na hata kila pembe zote za kenya. Kwa sasa anamiliki company yake mwenyewe ambayo inafayahamika kama Malindi Movie Magic. Medu ni mmoja kati ya ma video editor wanaofanya vizuri mjini Malindi. Big up Malindi Superstars

COAST ALL STARS LIVE SHOW

Image
Tarehe 20th jumapili pilkapilka zote zitakuwa mamangina drive pale wasanii wote wa pwani watapanda jukwaa moja na kuporomosha show moja ya kukata na shoka. Show hiyo inayowakumbuka watoto wa kike mkoani pwani imewaleta wasanii kama Dazlah,Kigoto,Shembwana,Shamaniz,NyotaNdogo,Ukooflani, Rudeboiz, Chikuzee,Pday, Alkenialuv, Rapdem,Kidis,Kaa la moto,Ohm's law, Odinareh, Vedette, Wynas, Lypso, Dogo richy, Vivonce....wooote watakuwepo!

KASSAMONEY:ITS MUSIC BUSINESS.

Image
WHATS YOUR STAGE NAME? Kassamoney Brian. WHEN DID YOU START DOING MUSIC?  I started The Rap Game When i was in High school.  WHO INSPIRED YOU MUSICALY?  50cent inspired me A lot... I Couldn't borrow or Copy everything from him because i too needed to be original.  WHAT TYPE OF MUSIC DO YOU DO?  I do Rap music. A music that moves the crowd.  WHERE DO YOU COME FROM?  Am from kongowea Kitaa Cha Biashara and that gives me more Potential ya kuwa kwa bizniz not just Industry For Fame.  SO YOU DO MUSIC BUSINESS UNLIKE MANY ARTISTES WHO DO MUSIC JUST FOR FUN AND FAME?  Yeah I'm In Music Business not Music Industry'  TELL US ABOUT YOUR MUSIC JOURNEY.  Kama Ujuavyo Mtoto Uzaliwa akakaa, Akatambaa akatembea then Mbio Yani kumake Steps iko Kila mahali Kwa Life i did so Many Track That Didn't do Well. I went To Nairobi and did a Ghipuka Track At Pacho Ent. Wit CALTOZ JINAMIZI... But still things didn't go well. I came bac...

BROTHERPEACE: "SIHITAJI MAPENZI NA SITAKI KUSUMBULIWA

Image
" Mkali wa miondoko ya mduara na mambo ya kiswazi BROTHERPEACE amekuja wazi na kusema yanayomsibu.Mwanamuziki huyu ambaye pia ni mtangazaji wa kituo flani cha redios amesema kamwe hataki kusumbuliwa na mabinti kwa kutumiwa inbox na mabinti kila mara.Brotherpeace alikuwa na haya ya kunena........"Sihitaji mpenzi coz nimechoka kutongozwa kila Saa na wote hawana mapenzi ya kweli mpaka pale Mungu atanijalia mwenye kheri nami ndio nitakuwa naye lakini sio kwa sasa.........sina haja nao hata wanifuate vipi siwataki..." Habari ndio hio.

ANONYMOUS VEDETTE;I'M THE DEFINATION OF RAP!!!

Image
 JE ANONYMOUS VEDETTE NI NANI? Anonymous Vedette ni msanii anayeimba style ya hiphop. ULIANZA KURECORD MUZIKI LINI? Nilirecord my first song, mwaka jana katika Jungle Masters na producer Emmy D. JE WEWE HUPITISHA UJUMBE WAKO KIMUZIKI KWA LUGHA GANI? Mimi hurap na English sana, lakini pia naeza freestyle na kiswahili.  TUELEZE KUHUSU SAFARI YAKO YA MUZIKI. Nilikua mmoja wa wale wasanii waliowakilisha Mombasa katika competition ya Dont Break the beat alongside Kaa La Moto na Cypreezy na wengineo. KANDO NA MUZIKI WAJISHUGHULISHA NA NINI?  Kwa sasa niko Technical University of Mombasa nasomea Bachelors in Tourism Management. TUELEZE PROJECTS ZA MUZIKI UNAZOZIFANYA KWA SASA. For the past few months I have been working on self development and promotion so that The Anonymous Vedette can be a brand and not just a stage name. I however realized that it is hard to do that as an individual due to some factors. The way out is to work together and market our...