TISHIO KUBWA KWA SANAA YA AFRICAN MASHARIKI!!!!! MSANII HUYU MPENI HESHIMA ZAKE!!!!
Ni jina sifika Na tajika kwa sasa linalotikisa mawimbi ya muziki Afrika Mashariki huku washika dau wakiupiga muhuri Usanii wake Na saluti vilevile.
Beka the Boy anayetokea Malindi amekuwa gumzo kwenye majarida, gazeti, redio, mitandaoni Na ameleta mbwembwe kibao kupitia midundo yake iliyokolea utamu ya melodi nzuri nzuri za kuvutia.
Beka ukipenda Double B, amewika kwa vibao kama Niko low, siri ya Moyo Na inayovuma kwa sasa manenoz.
Video zake zenye uhai, mvuto Na picha zenye nakshi zinemuweka kwenye matawi ambayo wengi wa wasanii hawajafikia.
La kupamba zaidi ni kuwa jamaa huyu amekuwa kama bendera ya Pwani kwa sasa kwani ameingia ndani, ndani, ndani, ndaaaaaniiiiiiiii kabisaaaaa ya Afrika mashariki baada ya kupata airplay Na mahojiano kwenye redio za Tanzania Na Kenya vilevile. Redio hizi zikiwemo Sunrise Radio 94.9 FM iliyoko Arusha, Radio Jembe 93.7 FM Mwanza na Ice 99.5 fm ya Jombe.
Kwa sasa Beka the Boy yupo katika pilka pilka za kudondosha kibao kipya kwa jina "msanii" kilichoandaliwa Na produza Ammz wa Tempoz records.
Msikae mbali kwani Beka the Boy yupo tayari......
Comments
Post a Comment