RINGA TALEMO AWACHIA VIDEO MPYA AKIWAHIMIZA WASANII WAFANYE VIDEO ZAO NA WAAANDALIZI WA PWANI
Msanii Ringa Talemo Leo hii ameachia video yake ya Nipe Nipagawe chini Ya uandalizi wake produza Nau.
Talemo alirekodi wimbo wake ndani ya Thundersounds kwa produza Morbiz almaarufu Sherrif na akaamua kufanya video papa hapa Pwani.
"Nilionelea kazi hii nishughulikie hapa kwetu Pwani kwani waandalizi wa video wamekua wengi na wanajaribu sana kwa kazi zao.Kama wana uwezo kwanini tusikuzane sisi kwa sisi. Haina haja twende hadi Nairobi kufanya video ilhali Pwani kunao walio Na uwezo kama vile Produza Nau aliyedirect video yangu ya Nipe Nipagawe. " Alieleza Ringa Talemo kupitia njia ya simu.
Tazama video hapa Na uone kama imeweza ama bado
https://youtu.be/xGY5ALg0T8A
Comments
Post a Comment