SABABU KUU YA KIGOTO KUKIMYA KUFICHUKA!!!! SOMA HAPA!!!

Aliwika sana na kujizolea sifa kem kem kutoka kwa mashabiki sio wa Pwani bali Kenya nzima.
Tunamzungumzia msanii sifika Kigoto Mbonde. Staa huyu wa Kichapo cha Mapenzi alitoa hit kali kali zilizomfanya kuwa kipenzi cha watu.
Kigoto alifanya kazi studio kadhaa ila urafiki wake wa karibu sana ulikuwa kwa studio ya Produza Tk2,hapa tunazungumzia Hornet Records Na baadae Number one records.
Baada ya purukushani zisizoeleweka Kigoto alikatiza muziki ghafla na kunyamaza zii. Majuzi alirudi kupiga collabo Na Mswazi Masauti ambaye amenyamaza vilevile, nyimbo ikijulikana kama "Sawa." Cha kushangaza nyimbo hii haikupokelewa vyema Na ikabidi Kigoto kuingia mitini.
Meza yetu ya habari ilichukua jukumu la kuwasiliana na Kigoto kuhusiana na ukimya wake na hapo ndipo tulipobaini kuwa jamaa huyu alikua masomoni.
"Wajua mimi nilipomaliza shule ya upili, moja kwa moja nikaanza muziki hivyo sikupata nafasi ya kusoma. Sasa kupitia Wazazi ikabidi nitulize majembe yangu ya muziki na kurudi masomoni. Si wajua tena Wazazi wakinena lazima tuheshimu. Sijaacha muziki na kwa sasa nimemaliza masomo hivyo basi mashabiki watarajie muziki na burudani kwenda mbele. "Alieleza Kigoto.
Vilevile habari za chini Ya Maji zasema kuwa msanii huyu amepiga kolabo fulani ndani ya Tempoz records.

Comments
Post a Comment