NITAWALIPISHA WASANII WA PWANI WAKITAKA COLLABO - MSANII ASEMA
Rapper anayetokea magharibi mwa Kenya, Noble Mirror amekua mwingi wa ghadhabu Na kutoa maneno ambayo tunaweza sema ni kama kejeli.
Noble Mirror anayejiita Mwamba wa Magharibi alisema kuwa wasanii wa Pwani pamoja Na maproduza hawajui lolote Na wakati umefika waambiwe ukweli.
"Kati ya wasanii ambao hawajui wanachokifanya ndani ya tasnia hii ya mziki ni wasanii kutokea mombasa na baadhi ya producers wao.
Mfano , Mimi nikiwa katika tour zangu Coast nimewai kutana na wasanii na producers kadhaa wakaniomba collabo nikakubali kiundugu na pia tukapiga kazi Kali tu.
Kati ya kazi nilizopiga nao niliwasihi nizipeleke Nairobi kwa producers wazuri zaidi kisha zifanyiwe mixing nzuri ila wote waliishia kukataa na mwishowe kupiga mixing mbovu.
Hii inafanya niwatolee macho wasanii wa coast kali na kuwalipisha collabo ndio mwisho wa siku awe na bidii ya kuingiza kazi kwa soko.
Kuhusu producers nitakuwa mkali sana kwa yeyote anayefanya kazi ya sauti yangu ju najielewa Sana na pia nina sauti ya BEI KUBWA." Alisema Noble Mirror.
Comments
Post a Comment