SHINEY ANNE ARUDI TENA KWA WIMBO WA AMANI


Huku Pwani ikizidi kudorora kwa wasanii wa kike, msanii Shiney ameamua kurudi kimuziki.
Shiney Anne, aliyevuma kwa vibao vikali vikali kama ride on me, ilingi, kilio Na vinginevyo alizima ghafla na kupotea kwenye ukumbi wa sanaa.
Tulijaribu kuwasiliana naye Na alikua Na haya ya kutueleza,

"Sio kuwa nilikimya kwa ubaya ama kwa kushindwa na muziki ila majukumu kadha wa kadha niliyafuatilia na pia nilitaka kuchukua break ili niweze kusoma huu muziki vizuri zaidi. Hata shule pia huwa kuna vipindi vya mapumziko. Hivyo basi mimi pia nilikua kwenye kipindi cha mapumziko na kwa sasa nipo tayari asilimia moja kuwapa burudani, kuhamasisha jamii na kuwa kielelezo chema kupitia muziki. "

Shiney kwa sasa yupo matayarishoni ya kuachia kibao kipya kuhusu amani. Wimbo huo umetayarishwa na produza Baindo chini Ya Bigfoot production Na utawachiliwa rasmi tarehe moja mwezi wa Agosti.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA