HAKUNA KUNDI LA KUTUTISHA - YAKWETU BAND YAAMKA!


Band ya muziki ya Yakwetu imeamua kuleta vurugu kwenye ukumbi wa sanaa.
Band hii iliyotambulishwa na produza Ammz baada ya kutoa kibao chao Olele na kuingia mitini imerudi kwa kishindo kwa kazi mpya kabisa.
Baada ya kuwasiliana na kundi hili, Yakwetu walitueleza kuwa kwa Mara ya kwanza walikua wamekuja kutazama tu Sanaa Na kufanya upelelezi kuhusu muziki wa Pwani Na wa Kenya kwa jumla.

"Tulikua tumeambiwa kwamba muziki hasa hapa Pwani ni mgumu mno kwa hivyo tukaamua kuyajaribu maji ya sanaa tupime kimo chake Na tulipogundua kwamba tunao uwezo basi sasa ndio kazi imeanza rasmi. Tulidhani Kuna wakali kutuliko sisi ila hataa..... Pwani hakuna wa kututisha na wimbo wetu mpya Sugar lazima utaingiza hela Nakutuvusha hadi ng'ambo ya Afrika mashariki. "Alieleza mmoja wao.
Wimbo wao Sugar umeandaliwa Na produza Ammz ndani ya Tempoz records Na hivi karibuni mtauskia. Yakwetu ni ya Kwetu kweli!!!!!!

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA