YAKWETU BAND : ISINGEKUWA LIZZ JASOLJAH BASI TUSINGELIJULIKANA!
Band inayopeta kwa sana tu, Yakwetu Band imetoboa siri ya mafanikio yao.
Kikundi hiki kilichoanza anza mbwembwe zake mwaka uliopita 2016 kimemtaja Lizz Jasoljah kama msingi wao wa kutoka kimuziki.
"Kusema ukweli ule, isingelikua Lizz basi tusingefika tulipofika. Manake tulipojuana naye ndio mambo yetu yalianza kufunguka na yuyu huyu Lizz ndiye aliyetupeleka kwa producer Ammz na tukarekodi ngoma kwa jina Olele. "Walieleza vijana hao.
Yakwetu, ilipata umaarufu wa haraka jambo lililopelekea wao kuchaguliwa kama nominees wa Pwani Celebrity Awards. Kwa sasa ngoma yao ya ''sugar" ipo hewani na inafanya vyema Sana.
Comments
Post a Comment