MSANII MASHUHURI AVULIWA VIATU KISA NAULI YA BODABODA!!!!
Msanii MASHUHURI AVULIWA VIATU KISA NAULI YA BODABODA!!!!
Ni tukio la kutamausha lililotokea hivi karibuni pale msanii aliposhikwa matai na kuvuliwa viatu hadharani.
Kisanga hiki kilitokea juzi mitaa flani ya Mariakani baada tu ya sikukuu za Iddi.
Meza yetu ya habari ilibaini kuwa kalameni huyo ambaye ngoma zake hasa hupigwa kwenye disko vumbi na disko matanga aliabiri Bodaboda Na kuahidi kumlipa mwenyewe vinono pindi atakapopiga show kwenye tamasha flani la disko vumbi. Msanii wetu aliingia mitini Na kuvunja ahadi Yake ya kulipa nauli.
Baada tu ya wiki moja, gwiji wa disko alijipata matatani pale mbio zake za sakafuni zilipoishia ukingoni Na kupatikana mitaani akiranda ovyo. Hapo ndipo alipobaini kuwa siku za mwizi ni arubaini. Jamaa wetu alibamizwa makonde ya mbavu Na kuvuliwa viatu..........WASANII BANAE!!!!
Comments
Post a Comment