PRODUCER WA PWANI AFUNGUKA MENGI KUHUSU SANAA YA PWANI. SOMA ZAIDI HAPA!
Produza msanii Lameck Boy wa Neptune records alifunguka mengi kuhusiana na sanaa ya Pwani hapo jana,25th. 7.2017.
Lameck Boy aliongea haya baada ya kuona msukosuko flani ndani ya dau hili la muziki wa Pwani. Tukinukuu....
" Sanaa ya Pwani kikweli iko na muziki mzuri,ambao mtu anaweza penda kuusikiliza nakuushabikia,wasanii wako wenye bidii,maproducer wazuri pia,watangazaji pia wazuri wanaosapot muziki.Wako wasanii tajika kama Susumila,Ally B,Nyota Ndogo,Chikuzee,Sudi Boy,Dogo Richie,Fat S,Fisherman,Escobah,Simon Simz na wengine,wako maproducer tajika,nikiwemo,akiwa pia P Baindo,Amz,Emmy Dee,Toti,Noor Mwamba,Tk2,J Crack,Lai,P Lion,Mobiz na wengi ambao tunafanya kazi nzuri.
2;Vitu ambavyo vinaweza au vinarudisha nyuma sanaa ya Pwani ni vitu vitano.... "
1. Wasanii kutopendana,kutofanya kazi pamoja,wasanii kujiona bora kumliko mwengine.
2. Maprodusa pia kukosa kuja pamoja nakushirikiana,wengine kujiona wao ndio wakali kuliko wengine,produsa kujifanya anajua kila kitu,kiburi.
3. Baadhi ya watangazaji kutopeana full support kwa kazi za wasanii wanyumbani,aitha chipukizi au hata aliyebobea,wanapeana sana promo kwa wasanii wa nje sana kwa kifupi,wanajenga kwa jirani kwao wanaacha kukivuja,na pia watangazaji wengine wanaangalia tu kazi za maprodusa waliowazowea badala yakuangalia upcoming producers wengine wanafanya kazi nzuri hata kuliko waliobobea.
4. Ma meneja kutokuwa serious na wasanii,wanataka kufaidika wao peke yao bada yakufaidisha hata yule msanii,shows hawatafuti nje ya pwani,hawa market wasanii wao vizuri,radio na tv,video poor quality.
5. Shabiki kutoitisha nyimbo za wasanii wao ,wanaitisha sana nyimbo za nje.
. Sanaa ya pwani sio changa,ila watu huitafutia sababu zakuiweka changa kila siku,kwa kuilenganisha na sanaa za nje,ambapo nchi kama bongo,uganda,naija, kule wamethamini sana wasanii wao nakuwaenzi,nakuusukuma muziki wao hadi huku umetambulika,ambapo sisi hapa pwani hatufanyi hivyo.watu hukimbilia nairobi,au bongo wakiamini ndio kutoka,sio kweli,wako wasanii wa nairobi wamejulikana bila kukimbila pwani,bongo na kwengine,na wapo wasanij hapa kwetu pwani ambao wametambulika bila kukimbilia nairobi au bongo.
Kile kitu naweza sema nikuwa tuupende mziki wetu,kama ni m'baya tuueekebishe wenyewe hadi uimarike kama wengine badala yakuuponda,nakuukejeli,haisaidii,wasanii tuache kulalamika tujitume tutafute shows,tutafute radio n tv interviews tuusambaze muziki wetu,tuache kujikweza,tuache kupondana ,tuache sifa natufanye kazi zionekane sio mijisifa yakijinga mitandaoni.
Akimalizia produza huyu alitia himizo kwa wakenya wenzake,mashabiki,wasanii,maproduza Na watangazaji,waishi kwa amani,wapige kura kwa haki na kweli. Na kwa mashabiki zake wasubiri vibao vikali kutoka kwa studio yake NEPTUNE RECORDS,pindi tu baada ya uchaguzi mashambulizi yataanza.
Comments
Post a Comment