RAPPER ALIYEAMUA KUKITA MIZIZI KABISA, KOFFI MACHETE!!!!!!! JE BIFU YATOKOTA KATI YAKE NA NASSIZU AU KRISTOFF???


RAPPER ALIYEAMUA KUKITA MIZIZI KABISA, KOFFI MACHETE!!!!!!! JE BIFU YATOKOTA KATI YAKE NA NASSIZU AU KRISTOFF???

Koffi Machete  ndilo jina tajika kimuziki kwa sasa hasa pande za Meru,msanii huyu ambaye mashabiki wengi wake wamemkubali kwa mtindo wake wa kufoka amekuja Juu pale wimbo wake aliotoa majuzi kudhihirisha ushindani na beef kati yake na msanii mwenza wa Meru Nassizu.

Huku akifanya kazi Na wasanii tofauti tofauti wanaofanya vizuri pande za Meru jamaa huyu amedhihirisha Na kujikaza mkanda Na vibao vyake vitatikisa Afrika Mashariki kwani muziki wa rap umemvaa vilivyo.

Gwiji huyu amefanikiwa kufanya nyimbo na msanii tokea Mombasa sudi boy uliompa umaarufu sana licha ya Sudiboy kudinda kuuongelea.
Zaidi amefanya nyimbo kadhaa mwaka huu zikiwemo Village boy,Machete Na nyinginezo  zilizompa umaarufu sufufu.Vilevile akafanya video yake ya wimbo 'moto' iliyoandaliwa  na Steve Kipande . Kwa sasa Koffi Machete amedondosha kibao kwa jina Dogodogo pamoja Na video yake yenye viwango vya juu iliyotengenezwa Na mkali Johnson Kyalo.Vilevile habari za chini Ya kapeti zasema kuwa rapper huyu Kuna vile amemdiss Kristoff kwenye wimbo wake mpya.

Tulipata kuwasiliana Na mshika dau mkuu wa sekta ya muziki Meru ambaye vilevile ni mmliki wa Lebo ya Watanashati, Kayfar, Na akatupasulia haya,
"Muda huu huyu jamaa anakuja vizuri na mimi Kayfar ,kama marketing manager wake pamoja na manager wake Doreen tunadhibitisha kwamba muda huu tutamuweka kwenye level za juu za kutamanika hata na wasanii wengine.Zaidi ni performer mzuri sana na amefanya baadhi ya show kubwa kubwa nchini haswa Meru. "

CHEKI VIDEO YAKE HAPA----->>>

Dogo Dogo - Koffi Machette x Rangeh [Officia Musi…: http://youtu.be/faaqXy9FU90

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA