MSANII WA PWANI AFURA TUMBO KISA DENI KWA MGANGA!!!
MSANII WA PWANI AFURA TUMBO KISA DENI KWA MGANGA!!!
Bila shaka ni matukio ya kutamausha yaliyojiri juzi usiku kuamkia Jana pale msanii alipofura tumbo mithili ya mja mzito wa pacha.
Msanii huyo tutakayembana jina kwa sasa(kuzuia aibu) alianza kuumwa na tumbo kuanzia juma lililopita na maji yalizidi unga pale alipoamka usiku na kujipata na kitambi cha lazima.
Inakisiwa kuwa kalameni huyo anayetokea mjini Mombasa alitamani umaarufu wa haraka ndiposa akafunga safari hadi sehemu iitwayo Vigurungani,kaunti ndogo ya Kinango na kukutana na mganga kwa jina Mzee Chikophe.
Babu huyo alimfanyia ganguzi zake na akampa ada ya shilingi elfu tano.
Msanii alimlipa mganga shilingi elfu moja na kuahidi kumaliza masalio yake kwa juma moja.
Baada ya kutoikamilisha 'promise' yake kwa juma moja basi shida ndipo ilipoanza.
Msanii wetu huyu aka Bin Kitambi alisifika kwa nyimbo kama vile PENZI LAKO,SAUMU,UTULIVU WA MOYO na DISKO KALI zilizopigwa sana kwenye sehemu za disko matanga,harusini,mangweni na hata katika baadhi ya vituo vya redio hapa pwani.
Comments
Post a Comment