KAMA WEWE UPO QATAR BASI HII NI YAKO!!! TOKA MOMBASA HADI QATAR!!!


Baada ya kuwaangazia wasanii waliosafiri kwenda uarabuni kwa minajili ya kazi,meza ya habari ya Pwani Usanii imebaini kuwa wasanii fulani wamekuja pamoja ili kuweza kuendeleza vipaji vya wasanii wanaofanya kazi Uarabuni.

Wakiongozwa na msanii MNS,wasanii walio nchi ya Qatar watafaidi kabisa kwani organisation hiyo kwa jina TEAM RIYAL TALENTS ipo chonjo kushika mkono kipaji chochote cha msanii anayefanya kazi sio Qatar pekee bali nchi yoyote ya Uarabuni.
"Tumefungua like an organisation tunaiita TEAM RIYAL TALENTS ambayo tuko Na connection za studios huku Qatar kama "RECORD ON STUDIOS Qatar" Na "BIGFOOT PRODUCTION" Kenya.Ambapo wasanii walioko huku wanaweza pata fursa ya kuendelea na Mziki ijapokuwa hawapo Kenya." Alieleza msanii MNS.
Kwa Sasa TEAM RIYAL TALENTS wamerecord wasanii kadhaa kama,RIO D ,PRINCE,MEJAKALZ na MNS WA KWETU.

Nyimbo za wasanii hawa zitaachiliwa rasmi hivi karibuni kupitia ukurasa rasmi wa Facebook unaoitwa "Team Riyal talents".
Mns kupitia mahojiano kwa njia ya simu aliwapa mashabiki hakikisho kuwa vipaji vipo na kamwe havitapotea kamwe.
Mns aliongezea haya,"Team Riyal Talents ni hope ya wale wenye vipaji ambao wapo Qatar,Mimi ndio muanzilishi na nimesign wasanii wawili ambao Ni prince Na Mejakali.Nia yetu Ni kuinua vipaji vipya Na hata vile vishachipuka tayari
Na kuondoa wazo la kuwa msanii akishasafiri hasa Uarabuni ameacha muziki."

Kwa sasa wasanii wasubiri kibao SWEETY BY MEJAKALZ FT PRINCE and MNS WA KWETU.Vilevile Kwa wasanii walioko Qatar wanaweza kuwasiliana na MNS kupitia email hii Nasirsalim61@gmail.com .

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA