HIVI JE HII NDIO NEMBO MPYA YA MOMBASA KAUNTI??!




Baada tu ya kuangusha wimbo wao KARIBU MOMBASANI, wasanii Benso,Kigoto na Gee Gee wameonekana sehemu tofauti wakieneza injili ya wimbo wao.
Kumbe tusilolijua ni wimbo huu ulitengezewa nembo na wasanii hawa kupitia wizara ya vijana ya kaunti ya Mombasa wamepewa idhini kuzuru kila mahali panapovutia watalii ili kuweza kupiga picha nembo hiyo hapo.



Vilevile ofisi zote za kaunti ya Mombasa za wizara yoyote ile,wasanii hawa wamepewa msukumo na kipao mbele kuingia na kuweka muhuri wao kwa kupiga picha na nembo hiyo ya wimbo Karibu MOMBASANI.



Pia,wizara ya vijana imeahidi kufanya kazi na wasanii hawa watatu kupitia nyimbo yao ili kuweza kuwakaribisha wageni,kuukuza uchumi wa Kaunti ya Mombasa na kuongeza vijana ajira.



Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA