PRODUZA BILLY MOYSES ARUDI KIMUZIKI NA KUTAMBULISHA KUNDI LA WATOTO.
Produza aliyevuma kwa kibao mtazamo.Billy Moyses baada ya kimya kingi ameamua kuzivaa njuga na kurudi ulingoni. Produza huyo aliyemiliki studio yaNewdawn records alipotelea masomoni kwa mwaka mmoja.
“Nilikuwa naongeza ujuzi zaidi na vilevile kutafuta vyombo vya kisasa vya kuandaa muziki.” Alieleza BillStudio yake kwa jinaBaraka music imefunguliwa rasmi na Produza huyu yupo tayari kufanya kazi na msanii yeyote.
Vilevile,ili kuregesha shukrani kwa jamii,Billy Moyses amewachukua watoto mayatima nakutengeneza bendi nao.Watoto hao wanaotoka orphanage yaLIKONI AIDS ORPHANAGE watarekodiwa album moja bure na kufanyiwa marketing. Pesa zitakazo patikana kutoka kwa kazi hiyo zote zitaenda katika elimu ya watoto hao.
Bendi hiyo ya watoto watano yafahamika kama LAOP MELODIES na tayari washawachia kibao kipya PARADISO.
Comments
Post a Comment