AKOTHEE AVUNJILIA MBALI HARUSI YA PILI!!!!!?????
Mwanadada anayetamba kwa kasi Afrika Mashariki Akothee alipasua mbarika hapo jana kuwa hataki tena mambo ya ndoa na harusi.
Akothee aliyejizolea tuzo majuma mawili yaliyopita kwa wimbo wake Sweetlove akimshirikisha Diamond alieleza haya wakati wa mahojiano kwenye kipindi cha THE TREND cha LARRY MADOWO.
Akothee alimwaga mtama penye kuku wengi aliposema kuwa mumewe yuamsumbua kwa kutompatia wakati wa kuwa pekee na kumzua kufanya mambo yake kibinafsi.
"Amekuwa hataki niende show muhimu,mara anadai kuwa nafanya muziki burudani muda mwingi na akaniambia nichague muziki au yeye.Mimi nikachagua muziki." Alieleza Akothee.
Comments
Post a Comment