PATA KUMFAHAMU MSANII PRINCE WA KIKOSI CHA TEAM RIYAL TALENTS.
Kwa majina kamili ni Samir Said na jina la usanii anafahamika kama Prince.
Msanii huyu aliye chini ya himaya yake msanii MNS,ndani ya lebo ya Team Riyal Talent alianza usanii kitambo kidogo wakati alipokua shule ya upili.
Enzi hizo, Prince alikua gwiji wa tamasha za muziki na michezo ya kuigiza shuleni kwao (Kenya music and drama festivals).Akiandika na kuelekeza mashairi hadi Kiwango cha kitaifa.Mwaka wa 2006,Prince aliibuka mshindi kwenye ulingo wa ushairi katika kitengo cha kitaifa.
Msanii huyu anayefanya muziki wa kipwani vilevile hufanya mitindo ya rnb,afro-fusion na trance.
Prince ameandaa kibao kipya kabisa akishirikiana na Msanii Mejakali na MNS. Wimbo huo kwa jina 'Sweety' utadondoshwa hivi karibuni.
Studio za RECORD ON STUDIOS QATAR na BIGFOOT PRODUCTION ndizo zinazomsaidia Prince kunoa makali yake kimuziki.
Producer Lee wa Qatar humpa wakati msanii huyu kupiga tizi na kumhimiza kujikaza kisabuni huku Produza Baindo akimtengezea midundo ya kimwambao.
Kinachomtia shinikizo na motisha msanii huyu ni kuwa anajijua ana kipaji na lazima afanikishe malengo yake kimuziki.
"Kipaji changu ni muhimu sana na nisipokiangalia na kukifanyia kazi bila shaka kitapotelea mbali na hilo sio jambo la busara.Ndiposa nikaamua kujitosa ndani ya maji yenye kina kirefu na kusawazisha ari yangu kwa sanaa." Alituleza Prince.
Prince vilevile anataka kusaidia wasanii wasiojiweza na wenye vipaji ili waweze kujikimu maishani kupitia muziki.
Msanii huyu amewahimiza wasanii wote walio pande za Qatar kuweza kujiunga na kusupport Team Riyal Talents.
Indeed he is one in a million...
ReplyDeleteAmazing n very inspiring...all da very best prince...sky is da limit
ReplyDeleteOnce in a lifetime kinda man n friend
ReplyDeleteSimply superb❤