HUBA MAHABA! MSANII DULLY MELODY KUMBE MPENZI WA RAPPER CML??
Chambilecho wahenga,mapenzi ni kama kikohozi hayafichiki,hivyo basi msanii Dully melody ameamua kumwaga mtama waziwazi penye kuku wengi.Dully alizimwaga hisia zake kwa mwanadada CML mwanamziki wa Hiphop kutoka mkoani pwani.Msanii huyu wa kibao cha YAGAYAGA ameeleza kwamba anavutiwa na vitu vingi vilivyopelekea yeye kumpenda...
"CML ni mrembo sana,wengi wanatamani kuwa naye ,hana dharau,wala kiburi.Ana uwezo mkubwa kwenye gemu,napenda kazi zake na zaidi ana roho safi sana.Sijasikia amegombana na mtu au ana bifu,"alitudokezea Dully.
Ukaribu wao ndio uliochangia uhusiano wao kukuwa na kuamua kuwa wazi katika mitandao ya pasipo kuogopa.Hii ni baada ya wawili hao kuonekana Ukunda wikendi iliyopita na baadhi ya watu kuzungumzia.
Kutoka upande wa CML ,ambaye ni MSANII wa kike anayefoka ajabu na anayesifika kwa kibao chake cha 'Bao nishafunga',haikua rahisi kupata jibu lake kuhusu uhusiano huo kwani hivi ndivyo alivyosema,
"Love is a beautiful thing and every woman wishes to find a good man.Dully is a nice guy.Mimi Napenda kubembelezwa na kupendwa vizuri,na zote amejaliwa.siwezi ongea mengi kwa sasa,ila jibu mtapata kwani mapenzi hayafichiki."
Comments
Post a Comment