MFALME WA SWAHILI RnB AWAFYATA VILIMI WASANII WA PWANI!!
Zungumzia vokali zilizotulia na ustadi wa sauti na hapo hutokua umekwenda kombo kwa kumtaja msanii Dodger Rnb.Msanii huyu aliyechipuka miaka michache iliyopita kwa kibao chake 'Fall in Love' tutakua hatuwavishi kilemba cha ukoka tukimpa taji la 'Mfalme Wa RnB Pwani.' Wa kutupinga nani?
Alipoachia wimbo wake 'poporipo' uliotikisa chati si za pwani pekee bali pia nchi jirani ya Tanzania,Dodger RnB alijizolea mashabiki kibao waliokubali ustadi wake wa hali ya juu.
Jamaa huyu aliyejaliwa na ushairi wa mahaba amewachia video mpya akimshirikisha rapa Rahollic.Sio kuwa Dodger amebahatisha bali amewafyata vilimilimi wanaojibandikiza vyeo vya ufalme wa swahili RnB. Tazama video yake chonjo ya wimbo kwa jina 'Lullaby' iliyotayarishwa na Fishbone entertainment
https://youtu.be/sBYRwvwAgPw
Comments
Post a Comment