WASANII CHUNGENI SANA NA HUYU JAMAA
Majina yake kamili ni ABUBAKAR JUMA,ila jina la usanii ni NORRY CLASSIC.Norry alizaliwa tarehe 2 mwezi wa pili mwaka wa 1995.
Msanii huyu anayefanya muziki wa RnB alilelewa Mtwapa na kusomea shule mahali tofauti tofauti hapa Pwani.
Ni mwaka wa 2009 ndipo bingwa huyu wa kiswazi alipojiunga na kikundi cha muziki kiitwacho WEST NORRIEGO cha watu watatu.
" Tulitoa wimbo wa kwanza uitwao SUBIRA chini ya producer Lil I,Tino,ambaye ndiye CEO wa WAPISHI MUZIK studio iliyopo Mtwapa."alieleza Norry.
Kwa usemi wake mwenyewe Norry alisema kuwa aliyemkuza sana katika ulingo wa sanaa ni Produza Tino.
"Tino amenikuza amenilea kama mwanawe katika muziki hadi hapa nilipofika,vilevile nimepitia changamoto nyingi katika muziki ila rafiki wangu wadhati ATUMIK WALEO A.K.A ABELO amenipa sana moyo na kunisupport katika muziki hadi hapa nilipofika," alieleza Norry.
Akiwa mtoto wa kiume wa pili katika familia ya watoto saba ya Mzee juma,babake hakupenda Norry aimbe alitaka asome kwa bidiii shuleni kama kila mzazi anavyotaka.
Japo hakuwa mzuri sana katika masomo,mzaziwe wa kike kwa jina Everline alimpa moyo.
"Maisha ya shuleni niliyaona magumu nilitaka nimalize niendeleze kipaji changu,wakati nilipokua darasani mwalimu akifunza kwangu ilikua nadra sana kusikiliza mwalimu,vitabu vyangu vyote vilikua vya mistari tuuu." Alisema.
Kwa sasa Norry Classic yupo chini ya studio ya Wapishi records iliyopo Mtwapa na ameachia nyimbo kwa jina NINAVYOMPENDA na nyimbo yake ya Pili TELEPHONE NUMBER ipo njiani.
Comments
Post a Comment