MSANII APL JENNA:KUTOKA MTWAPA HADI NAIROBI KUENEZA INJILI KUPITIA MUZIKI.
Ni binti aliyejizatiti kueneza injili ya Kristo na kuwateka kondoo waliopotea kuwarudisha zizini. Msanii Apl Jenna anayetokea Mtwapa ila kwa sasa yupo Nairobi kwa mara ya kwanza kabisa ameachia video yake kwa jina HALELUYA.
Wimbo huo ulitayarishwa katika studio za MAINSWITCH na tayari unafanya vyema kwenye ulingo wa muziki wa gospel jijini.
Msanii huyu ameshawahi piga show kubwa kubwa kanisani,kwenye mikutano ya injili na show za kuandaliwa vilevile.Huku akiwa bado mchanga kwenye ulingo wa muziki,Apl Jenna amewapa hakikisho mashabiki kuwa ataeneza injili na kumtukuza Mungu kupitia muziki ili malengo yake yatimia.Pata kuitazama video yenyewe hapa.
https://youtu.be/cBEMz40NJCY
Comments
Post a Comment