EXCLUSIVE INTERVIEW:ONE ON ONE NA BINTI MREMBO APL JENNA!
PWANI USANII:JE,WAFAHAMIKA KAMA NANI?
JENNA:Naitwa Jenna Wangechi Apollo ila jina Langu la kisanii ni Apl Jenna.
PWANI USANII:UNATOKEA PANDE GANI YA KENYA?
JENNA:Nimezaliwa Nairobi nikasomea kuko huko kisha nilipomaliza kidato cha nne nikarudi Mombasa,Mtwapa kuishi na familia yangu.
PWANI USANII:MBONA UKAAMUA KUFANYA MUZIKI WA GOSPEL?
JENNA:Kwanza kabisa mimi ni mcha Mungu Vilevile wazazi wangu wamenilea katika mazingira ya kumcha Mungu,hivyo siwezi kamwe kwenda kinyume nao ndiposa nikaua kutumia kipaji changu cha muziki kueneza injili pekee.
PWANI USANII:UKO NA UMRI WA MIAKA MINGAPI?
JENNA:Nina umri wa miaka 20.
PWANI USANII:ULIREKODI WIMBO WAKO WA KWANZA LINI?
JENNA:Nilirekodi wimbo wangu Haleluya mwaka huu January na Mainswitch production) ambapo ulikua wimbo wa kwanza.Nilirelease mwezi wa tatu.
PWANI USANII: WIMBO WAKO HALELUYA ULITAKA KUPITISHA UJUMBE GANI?
JENNA:Ujumbe mkuu wa nyimbo 'haleluya' ni Kumshukuru Mungu kutokana na wema wake kwangu.
PWANI USANII:HIVI USHAWAHI FIKIRIA KUFANYA MUZIKI WA KIDUNIA AMA SECULAR?
JENNA:Watu wengi hunisukuma kufanya nyimbo za kidunia kutokana na urembo wangu,hataa hivyo maadili na msingi wangu ni tofauti sana.Kamwe siwezi kubali kufanya secular.
PWANI USANII:LENGO LAKO KUU NI LIPI KWENYE TASNIA YA MUZIKI?
JENNA:Lengo langu ni muziki wangu kufikia watu tofauti,na pia kupitia huo mziki waweze kubadilika.Niliamua kuchukua mkondo huu tofauti kuonyesha sisi vijana kuwa tusifanye vitu ili tufurahishe walimwengu.Ni vyema kutumia vipaji vyetu kumtumikia Mungu na kusaidia jamii.
PWANI USANII:KANDO NA MUZIKI UNAJISHUHULISHA NA NINI?
JENNA:Bado nasoma nipo Chuo kikuu cha Mombasa (TUM).
PWANI USANII:KITU GANI KINACHOKUPA MSUKUMO MKUBWA KUWEZA KUENDELEA MAISHANI?
JENNA:Mimi ni mtu wa maombi sana,kwa hiyo kila mara mi hupiga magoti na kumuomba Mungu aweze kunionyesha njia sahihi maishani.
Naamini sana msemo huu.Pray untill Something Happens....PUSH!
That's great,your music is inspiring and the potential inside of you is immeasurable and your destiny is greatness
ReplyDeleteThat's great,your music is inspiring and the potential inside of you is immeasurable and your destiny is greatness
ReplyDelete