NYOTA NDOGO KWENDA ULAYA KUPIGA SHOW KWA MARA NYINGINE!!
Mama mlezi wa sanaa ya pwani yaonekana ulezi umemkolea. Nyota Ndogo,ambaye hivi majuzi ameangusha video ya wimbo subira yangu, amedokeza kuwa yupo katika pilkapilka za kwenda nchi za n'gambo kupiga show.
Ni miezi kadha tu iliyopita ambapo Nyota amekuwa Germany akipiga show. Nyota aliyapachika maneno hayo kwenye akaunti yake ya Facebook na vilevile kuwashukuru mashabiki zake kwa kuupokea wimbo wake wa subira yangu vyema.
Comments
Post a Comment