***MOTOMOTO***SOCIALITES WA MOMBASA WAKABANA KOO!!!SOMA HAPA!!!!


Tukianza na Lil Kim Vs Nicki Minaj,Beyonce Vs Rihanna,Wema Sepetu Vs Zari the Boss Lady na Huddah Monroe Vs Vera Sidika .Bifu za mabinti zimezidi tokota kila sehemu na Leo hii twawaletea bifu la papa hapa nyumbani pwani.Kama kawaida,wanawake hupenda sana kuwekwa mstari wa mbele au kwa lugha ya kueleweka zaidi tuseme"kupewa attention" kuanzia majumbani,shuleni,mitaani,vilabuni,kazini na vilevile kwenye mitandao. Kasumba hii huleta migongono,lawama,wivu,Chuki na hata vita wakati mwingine.

Hivyo basi tukimwaga mtama penye kuku wengi, Ruthalia Michaels ambaye ni model,Emcee,Events organiser na video-vixen sifika hapa pwani yupo katika maji marefu na Gloria Kaychich ambaye ni model,business lady,Public figure,Video-Vixen etc.Wawili hao wamezua mtafaruku mitandaoni huku kila pande ikija na jeshi lake la kupigana vita vya maneno mitandaoni.

Huku wote wawili wakiwa na wafuasi wengi mithili ya siafu,Ruthalia alipachika maneno yaliyomkwaruza Gloria.Naye Gloria akijibu kwa hamaki bila ya kubembeleza.
Kuongeza msumari moto kwenye kidonda,mabinti wote wawili wapo kwa tuzo za Vibe City Awards Mombasa ambapo wamewekwa kitengo kimoja......,model of the year.Sasa macho mko nayo na kama u kipofu basi bila shaka utaelezewa utamu wa urembo wa mabinti hawa.Cheki maneno yenyewe kwenye picha kisha utajaza nani amemzidi mwenziwe!!!!!!

PICHA ZA RUTHALIA MICHAELS





PICHA ZA GLORIA KAYCHICH





WAWEZA KUWAPIGIA KURA HAPA---->>>MOMBASA VIBE CITY AWARDS---->>>https://contest.fbapp.io/vybe-city-awards-poll-eldoret-city-1331409

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA