ATI C'ZARS AMERUDI NA KATOA WIMBO MPYA ATAKAO UWACHLIA MWEZI HUU WA SEPTEMBER?
C'Zars ni jina sifika Afrika ya Mashariki,na hapa pwani limesifika sana. Mwanamuziki huyu aliyekua na bado yupo kinda wakati huo,alikua sukari ya watu wengi huku mashabiki wakimpenda na kukatika nyimbo yake ya AMKA UKATIKE.
C'Zars alionekana mara ya mwisho mnamo tarehe 13 Oktoba, 2006, na huo ndio wakati ambapo kipaji chake kilikuwa kimeiteka anga ya Afrika Mashariki. Amka ukatike ni wimbo wake wa kipekee alioufanya na uliwagusa wengi. Kipaji chake kiligeuka fahari kubwa kwa wazazi wake na vilevile wakenya kwa ujumla.
Ni takriban zaidi ya miaka kumi tangu aonekane na wengi wamejiuliza yuko wapi. Itakuwa vigumu kuruhusu akili kuamini kuwa C-zars yuko au anaishi sehemu fulani ya dunia. Ni binadamu gani anayeweza kujificha kwa zaidi ya miaka kumi? Maswali ni mengi ambayo yataulizwa ila majibu hayapo.
Awali uvumi ulienea kuwa kilichomfanya apotee ni woga wa mtihani. Kunacho kipindi fulani habari ilijitokeza kuwa Czars anaishi na mwanamke mzungu ambaye alimpa maisha ya kifahari japo habari hii haikuaminika. Mtangazaji maarufu wa kipindi cha Mambo Mseto Mzazi Willy M Tuva, alijaribu kuihoji familia yake nayo familia ilidai kuwa haina habari yoyote kuhusu uwepo wa mwanao.
Vilevile leo katika pitapita zetu,tulikumbana na blogi fulani iliyodai kuwa kuna uwezekano kuwa C'Zars yu hai. Cha kushangaza zaidi ni kuwa eti msanii huyu amefungua account ya Instagram na alipachika ujumbe kuwa amerudi na yupo na wimbo mpya kwa jina TANGU.Vilevile C'Zars inakisiwa kuwa aliwaambia mashabiki zake kuwa yupo tayari kabisa kuwapa burudani na wimbo huo ndio umeeleza jinsi maisha yake yalivyokuwa kwa miaka kumi alipotoweka.Kitambo kidogo wazazi wake walijaribu kutoa pesa nyingi kwa yeyote atakayetoa habari yoyote kuhusu pahali alipo lakini bado mbinu hii haijafaulu. Babake Abdulkarim Makasi alijitokeza tena hivi majuzi na kusema haya......
“WHEN HE COMES, HE CAN DECIDE WHERE HE WANTS TO LIVE. WE JUST WANT TO KNOW THAT HE’S WELL. ALL MY PROPERTY HAS BEEN REGISTERED UNDER HIS NAME SO FAR AND I HAVE BOUGHT A CAR FOR HIM TO USE WHEN HE COMES BACK. HE JUST NEEDS TO KNOW THAT HIS FAMILY STILL LOVES HIM AND IS WILLING TO SUPPORT HIM FULLY."
Blog tofauti tofauti zimeandika stori hii ya C'Zars ila ukweli wenyewe ni Mungu ndiye ajuaye.Yote tumwachie yeye Mungu muweza wa yote na kama kweli kibao kipya kipo basi itakuwa raha iliyoje kumpokea C'zars tena!
Comments
Post a Comment