KUTANA NA MSANII ANAYEIBUKA ANAYEMILIKI STUDIO NAIROBI NA MOMBASA.
Mula Sanz ni msanii anayetokea Mombasa ila kwa sasa yupo mjini Nairobi kwa ajili ya ajira.
Baada ya kugundua kipaji chake cha muziki akiwa shule ya upili,msanii huyu ajiunga na studio kadha wa kadha ila hakupata mafanikio.Ndipo akaangukia kazi ya shirika la Msalaba Mwekundu(Red-Cross) lililompa motisha wa kulisukuma gurudumu la sanaa
Mula,amefanya kazi kwa studio tofauti tofauti Nairobi na Mombasa zikiwemo; Mega Records,iliyopo maeneo ya Ngara na Hunters Records Mombasa.
Alipoona mambo yawamuendei anavyotaka,Mula Sanz alijitwika jukumu la kufungua studio yake binafsi na hivyo basi alinunua vufaa vya muziki vinavyohitajika na kuanza mradi.
Jamaa huyu alijipiga kifua na kuamua kufungua studio hiyo Nairobi ili aweze kurekodi wasanii wa jiji wanaotaka fleva za kimwambao.
Studio yake kwa jina Glashaz Records inapatikana Westlands Nairobi na vilevile Mtopanga mombasa pia ipo. Kwa hiyo Mula Sanz alifungua studio mbili ili kusaidia vipaji Nairobi na Mombasa.
Maombi makuu ya msanii huyu ni kufanya kazi na maproduza gwiji Afrika Mashariki na kutengeneza himaya yake binafsi kimuziki.
Vibao vyake maridhawa hupigwa sanasana stesheni kama Kbc radio Taifa,Bk radio na West Fm.Kazi yake mpya kabisa yajulikana kama NIMWIMBIE ambayo ni ya injili.
Pata kusikiliza baadhi ya nyimbo zake hapa.
http://mdundo.com/a/11406
http://www.reberbnation.com/q/6pftar
Comments
Post a Comment