MSANII MAN-AZZER YUPO TAYARI KUIPEPERUSHA BENDERA YA LAMU KAUNTI JUU!!!
Kando na kujaliwa kwa utamaduni uliokolea na mandhari mazuri ya kupunga hewa,Lamu vilevile ni nyumbani pa sauti tamu za kuburudisha na kufurahisha nafsi.Abbas Ali Shee ni msanii anayetokea Lamu na ameamua kuipeperusha bendera ya kisiwa hicho ili dunia iweze kuwatambua.
Jina la muziki anafahamika kama Man Azzer aliyezaliwa tarehe 23 mwezi wa September 1992.Msanii huyu mwenye sauti tamu mithili ya ninga alianza muziki tangu akiwa kinda.
Kadri miaka iliposonga,shauku yake ya muziki ilizidi ndiposa akaamua kujitosa mzima mzima kwenye bahari ya burudani.
"Niko kwa game huku nikiaminia iko siku Nitatoboa.Malengo yangu ya mziki ni kuwa na ndoto ya kuinua jina langu kwa wasionijua wapate nijua pia nipate mafanikio ya kusaidia familia yangu kwa jumla."
Alieleza Man Azzer.
Msanii huyu ambaye ndiye tegemeo kuu la familia yake hufanya mtindo wa rnb iliyokolezwa mahadhi tele ya kiswazi na ladha za utamaduni wa Lamu.Akiwa chini ya usimamizi wake Enoch wa IslandLove records, Man Azzer ashadondosha vibao motomoto akiwa na mwenzake Doni ambapo wamesajiliwa studio yiyo hiyo ya Islandlove records.
"Najipa moyo kuwa future yangu itakuwa poa na ndoto zangu kuziboresha kupitia muziki." Alisema Man Azzer.
Comments
Post a Comment