SIRI YAVUJA!!!! LIZ JAHSOLJA NA DULLY MELODY WAPATIKANA!!!!



Chambilecho wahenga,palipo na moshi hapakosi kuwa na moto. Staa wa kibao cha Yagayaga,Dully Melody amemwaga mtama penye kuku wengi. Dully, almaarufu Mr Yagayaga yaonekana pana uhusiano Fulani kati yake na aliyekuwa meneja au tuseme mpenziwe Dazlah,Liz Jahsouja au ukipenda kama mwenyewe anavyojiita Lioness.

Baada ya kutengana na Dazlah, binti huyu ambaye ni mwanaharakati na mshika dau mkuu kwenye tasnia ya sanaa ya pwani ameonekana sana akiwa karibu na Dully Melody. Kwenye kumbukumbu zetu kuna kipindi Fulani Dully alichora tattoo ya Liz kwenye kifua chake jambo lililoleta maswali mengi yaliyokosa majibu.

Walivyonena wahenga lisemwalo lipo na kama halipo laja basi mahaba yameanza kutokota na kuonekana waziwazi kwani tulipata kusikiza kidogo tu wimbo mpya wa Dully kwa jina tattoo ambao bado hajaumalizia na ni dhahiri shahiri kuwa anazungumzia Lizz.Kuongezea msumari moto kwenye kidonda,poster iliyotoka ya wimbo huo ina picha ya Lizz.Hivi nani alimpa ruhusa Dully kutumia picha ya Lizz kwenye poster yake.

Cha kushangaza,Lizz hajashare wala kuzungumzia kivyovyote vile wimbo RINGA wa Dazlah.
Yote tisa,kumi ni kuwa mapenzi ni kama kikohozi hayafichiki.Tusubiri wimbo wa Dully,tattoo tutapata majibu yote!!!!!

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA