YAKATOBINA VIDEO ITAFANYIKA EUROPE--JAFFARIZOH AWEKA WAZI MAMBO!!!


Ni msanii aliyekuja kwa wimbo Kali la kutikisa chati za muziki si wa pwani pekee bali Afrika mashariki kwa jumla.Msanii huyu mdogo kwa mwili ila mkubwa wa sauti wanajulikana kama Jaffarizoh. Jaffary kama wengi wamuitavyo alivuma kwa mara ya kwanza kwa vibao kama "mama Afrika" na "tell me" vilivyomuweka mahali pazuri kisanii.

Dogo huyu ameamua kuja kitofauti kabisa kwani mipangilio yake ya wimbo wake mpya YAKATOBINA imepangwa ikapangika.Jaffarizoh alitudokezea kuwa video ya wimbo wake mpya inaweza fanyika Europe.Japo hakutaka kutufafanulia ni nchi gani,msanii huyu anayerekodia Thundersound records aliahidi kuwa kwa sasa ataleta mapinduzi ya sanaa sio pwani bali Afrika mashariki. Kaeni mkao wa kula kwani YAKATOBINA video ipo njiani kutoka Europe.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA