PESA KWA PESA!!!MSANII JAGUAR AZUA BEEF MPYA NA AKOTHEE!!!
Hapa yaonekana ni pesa kwa pesa! Msanii tajiri Kenya Jaguar amezua beef mpya na Akothee.Jaguar anayevuma kwa vibao motomoto vinavyoshika chati si za Afrika Mashariki pekee bali Afrika nzima kwa jumla,alizua rabsha ya maneno wakati wa interview yake kwa kiss fm hivi majuzi.Msanii huyu ambaye vilevile ni mmoja wa wakuu wa NACADA shirika linalopigania umarufuku na utumizi wa vileo na dawa za kulevya,alimdharau sana Akothee kwa kumfananisha na Prezzo na kumwambia hana hela na hawezi lolote.Jaguar Alisema haya alipoulizwa na mtangazaji Shaffie Weru kama anaweza kufanya ushirikiano na Prezzo kwenye muziki.Jaguar alijibu hivi.......
"Unajua kudeal na huyu msee… I don’t know why kwa nini ananichukia hivyo. What I did when I was starting I told him yani… kuna watu walikua wamechukua industry ni kama ni yao like sisi watu wakutoka Eastlando we can’t enter. So what I did I told them unawezatoka uko Eastlands walikua wanaona chini na uwapite ata kama ni mababi.
So mi ntaachia Shaffie hio job aongee na yeye kwa sababu Prezzo ni mdifficult, tunaweza enda studio tena aanze mavitu haziko. Unajua ni male version ya Akothee. (akichekacheka)
Mimi simchukii Prezzo, namheshimu sana lakini akicome tufanye song aache hio mambo ya usocialite na akue mwanaume.”
Hivyo basi ni dhahiri shahiri kuwa Jaguar anamfananisha Akothee na Prezzo.Chuki na dharau yake kwa Akothee ni sawa kabisa na ile yake kwa Prezzo.Kaeni mkao wa kula kupata mambo yatakavyojiri,pwani usanii tupo kwa ajili yenu!!
Comments
Post a Comment