LO !! ILLUMINATI NA PRODUZA WA MOMBASA!!
Ameamua kuongelea swala nyeti linalogusia si muziki peke yake bali pembe zote za sanaa ulimwenguni.Produza Khalid a.k.a Eric Bizo,alifunguka kuhusu swala la illuminati kwenye sanaa.Khalid ambaye vilevile ni mmiliki wa A million records, studio tajika hapa pwani alipachika maandishi kwenye ukurasa wake wa fesibuku na kutaja vipengele Fulani vinavyohusiana na illuminati.
Tukinukuu baadhi yamaandishi yake,Khalid alikua na haya.....
"Ukiuliza mtu leo what's your desire...? utaskia "I want to be the best artiste in the world, I want to be the richest, I want to rule the world.... Etc" Sasa hilo ndilo swali watu huulizwa wakitaka kuingizwa kwenye 'Illuminati '.
90% ya wasanii wanaojulikana ulimwengu huu kutoka marekani ni Illuminati. Na kitu kilichowasukuma huko ni their 'desire' kuwa bora zaidi, tajiri zaidi, kwa njia ya mkato. Kile kitu watu hawajui ni kuwa Kuna 'rituals' au tambiko ngumu sana kwenye Chama hiki. Kwa mfano, ni lazima ukiwa mwanaume ufanye mapenzi na mwanaume mwenzako na muonyeshe watu hadharani. Kwa mfano Lil Wayne na Birdman wamekuwa wachumba kwa mda mrefu sana na kwenye tamasha kubwa kama BET na nyengine, wameonakana waki kiss hadharani.... Tattoo mwili mzima, kupiga picha za utupu, kutoa kafara, kunywa damu za watu etc Hivi ni baadhi ya vitu ambayo lazima uvifanye kudhibitisha wewe ni mwanachama.
Shetani alipewa mamlaka ya kutawala giza, kwa hivyo nia yake nikukutoa kwenye mwangaza. Atakupa utakacho kwa wakati mfupi 'in exchange of your Soul.' Wasanii waliojitokeza waziwazi kuwa 'they sold their soul to the devil' ni kama Rihanna, Beyonce, Kanye West, P. Diddy, Jay Z, Lil Wayne, Birdman, R. Kelly, Chriss Brown, Nicki Minaj etc... Filamu zote zilizo vuma lazima ziwe na ma "gay" au "Lesbians". Hii yote ni kazi ya shetani... Nia ya shetani ni kupindua hali halisi ya maumbile ya mwenyezi Mungu na kumkufuru... Na kwa
hili linawezakana kwa sekunde moja, ukimpa "Money, Power & Respect"
"What's Your Desire " hili ndilo swala nyeti. Shetani hapeani bure, lazima atakuuzia japo kuwa atakupa kwa haraka, na mwishowe atakupokonya ukikosea masharti. Michael Jackson, Prince, Tupac, Whitney Houston, hawa ni baadhi ya wasanii waliouwawa na Illuminati baada ya kwenda kinyume....
Ridhika na unachopata, punguza matamanio yako. Huwezi jua, lakini Wengi wanatamani ulipo. Mrudie muumba wako, yeye ndiye anayejua wakati gani bora wa kukupa, na akikupa hakupokonyi.... Tuwe na subra, tukiomba tutapata ila kwa wakati wake aliopanga Maulana..."
Comments
Post a Comment