UPUZI MTUPU !!! SUSUMILA NA KING KAKA WATOA VIDEO MBOVU-MAPEPE. HERI NISINGEIANGALIA!!!


Yaani baada ya kusubiri video muda huo wote matokeo ni ya haya??!! Tushabaini chanzo kuu cha wasanii wa Nigeria kupewa kipao mbele na media. Sasa jamaa hawa wawili Susumila na King Kaka/unaweza muita King wa video mbovu vilevile/ walikaa chini na kutuandalia video yenye very poor script-writing,poor location na dancers waliochanganyikiwa!!


Kando na hilo, storyline yenyewe haina hata mvuto ni kuboesha mwanzo hadi mwisho. Kilichoboesha zaidi ni hao wasanii wenyewe kuigiza ni kama wamekesha mangweni. Video yenyewe iliandaliwa na Empire pictures na Johnson Kyalo ambapo tukikumbuka vyema Empire Pictures ndiyo iliyoandaa video ya TULIZA NYAVU iliyokuwa mbovu na tukanyamazia. Hivi sasa, ati Mishemishe na Kaka ni Empires....!!! Vituko na vioja vilioje??? Empires zakutengeneza video zisizovutia?? Tafadhalini siku nyingine mkipiga collabo jaribuni kukaza kamba kidogo na kuumiza vichwa ili msiwabwage mashabiki.


Tazameni video yenyewe hapo..... https://www.youtube.com/watch?v=KUrnlMJEXGw/





Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA