MWANDISHI WA SANAA MANUEL NA RAPPER HUSTLA JAY WAZURU SHULE NA KUWAPA MOTISHA WANAFUNZI
Mwandishi mashuhuri wa gazeti na maswala ya burudani Manuel Ntoyai na mwanahiphop Hustla Jay,walitembelea shule ya msingi ya TIMBWANI Baptist iliyopo maeneo ya Likoni. Wawili hao walitembelea shule hiyo kama moja ya miradi ya AFRICA IS NOW FOUNDATION kuwahamasisha wanafunzi kuhusu maswala ya jamii,elimu na taaluma,talanta na maswala ya madawa ya kulevya.
Manuel ambaye ni kati ya wahariri wakuu na mwandishi wa sanaa na burudani wa gazeti la PEOPLE DAILY,majatida ya Spice na Tribe43 alikuja bayana na kueleza umuhimu wa utandawazi,elimu na taaluma naye Paul Maasai almaarufu Hustla Jay alizungumzia talanta na madawa ya kulevya mashuleni.
Wawili hao Vilevile,tulipiwasiliana nao walisema huu ndio mwanzo tu ila watazuru shule na kuhamasisha wanafunzi zaidi ili kuwasaidia kwenye safari yao masomoni.
Comments
Post a Comment