NYOTA NDOGO AFUNGA HARUSI(picha zipo)
Mlezi wa sanaa ya pwani,Nyota Ndogo hapo Jana alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wa kizungu. Harusi hiyo iliyofanyika hapo Jana mjini Voi ilikuwa na sheshe kibao japo baadhi ya jamaa na familia kutohudhuria. Nyota amefunga harusi na mpenziwe mwenye asili ya kijerumani na harusi yenyewe itachukua siku mbili.
Harusi ya Jana ilikuwa ya kidini na watu wa familia pekee na ya siku ya Leo (22,May,2016) ni ya kila mtu. Habari zinazotufikia ni kuwa ng'ombe kadha wamechinjwa kwa ajili ya sherehe hiyo na wageni pamoja na mashabiki zake Nyota Ndogo wamejaa furifuri kushuhudia na kusherehekea tukio lote.
Comments
Post a Comment